NA MWANDISHI WETU, DODOMA
MAKAMU
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Philip Isdor Mpango,
ameipongeza Benki ya NMB na kuitaja kuwa kinara katika kuunga mkono jitihada za
Rais Samia Suluhu Hassan za kupambana na Athari za Mabadiliko ya tabianchi.
Dk.
Mpango Ametoa pongezi hizo baada ya NMB kuzindua Kampeni ya Kitaifa ya Upandaji
Miti Milioni 1 kwa kushirikiana na Wakala huduma za Misitu Tanzania (TFS), huku
ikitenga kiasi cha Sh. Milioni 472 kuzizawadia shule zitakazofanya vema katika
shindano la utunzaji na uhifadhi wa miti.
Uzinduzi
huo sambamba na upandaji wa miti 3,000 ya matunda, kivuli, mbao na dawa,
umefanyika katika Mji wa Serikali, Mtumba, jijini Dodoma, hafla
iliyohudhuriwa na mawaziri, viongozi mbalimbali wa Serikali, Wadau wa
Mazingira, wanafunzi wa shule na Vyuo Vikuu, watumishi wa benki ya NMB
wakiongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna na Mwenyekiti wa
Bodi ya benki hiyo, Dk. Edwin Mhede.
Akizungumza
katika hafla hiyo, Dk. Mpango amesema kampeni hiyo chanya inaitia moyo ofisi
yake, na kubainisha kuwa kutokana na ukweli kwamba bila miti hakuna mvua,
chakula, maji, hewa safi na ndio chanzo cha mafuriko na athari nyingine za
Mabadiliko ya Tabianchi, Serikali inahitaji uungwaji mkono kama unaofanywa na
NMB.
"kinachofanywa
leo na NMB ni cha kuigwa na kupongezwa, kampeni hii inaenda kusapoti pakubwa
jitihada za Rais Samia, ambaye amejipambanua katika hili, amekuwa kiongozi
mwenye mkazo wa suala la mazingira tangu akiwa waziri, kisha Makamu wa Rais na
sasa akiwa Rais wa Tanzania, akitambua kuwa mazingira yanagusa sekta zote
kimaendeleo.
"Na
kwa mantiki hiyo, nasisitiza kuomba wadau wa mazingira, mashirika, kampuni,
taasisi na jamii kwa ujumla, kujitoa katika kumsapoti Rais Samia, kwani
Serikali Pekee haiwezi kufanikisha mapambano haya. Ndio maana naipongeza NMB
kwa uharaka wao kuitikia wito huo, zaidi kwa kuongeza fungu la Programu ya
Uwajibikaji kwa Jamii (CSR), sambamba na kubuni shindano la upandaji miti,
utunzaji na uhifadhi wa mazingira kwenye shule zetu.
"Kuna
maana kubwa kwa NMB kuongeza Shilingi Bilioni 2 kwenye CSR, ambazo ni maalum
kwa ajili ya mazingira, lakini kama haitoshi Ikatenga Sh. Milioni 472
kuzizawadia shule zitakazofanya vema katika shindano la upandaji na utunzaji
miti linalozinduliwa sanjari na kampeni hii. Zawadi za shule washindi ni nono
na kutokana na uwingi wake na idadi ya wanafunzi, maana yake elimu
inaenda kuifikia jamii kirahisi," alifafanua Dk. Mpango.
Awali,
akizungumza katika hafla hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth
Zaipuna alisisitiza kuwa athari za mabadiliko ya tabianchi hazijawahi kumuacha
yeyote salama na kwa kutambua hilo, benki yake ikaongeza fungu lake la CSR
kutoka Sh. Bilioni 4.2 (ambazo ni asilimia 1 ya faida yao kwa mwaka Sh. Bil.
429), hadi kufikia Sh. Bilioni 6.2, ongezeko linalothibitisha namna wanavyojali
na kuthamini mazingira.
Aidha,
akimkaribisha Makamu wa Rais, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano
na Mazingira, Mhe. Dkt. Suleiman Jafo alisema kuwa wizara yake iko tayari
kushirikiana vyema na Benki ya NMB na kuhakikisha kuwa adhma ya kupanda miti
milioni moja kwa mwaka 2023 inatimia kikamilifu.
“Wizara
yetu haitahakikisha miti hii milioni imepandwa lakini tutahakikisha miti hii
yote inkuwa na kustahimili ili iweze kuleta tija katika mazingira yetu na kuwa
na manufaa kwetu,” alisema Mhe. Dkt. Jafo.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali na Mitaa (TAMISEMI), Mhe.
Angella Kairuki alimuhakikishia Makamu wa Rais kuwa wizara ya TAMISEMI
watahakikisha uratibu wa mashule katika shindano lililoasisiwa na Benki ya NMB
unaenda kiufasaha na shule nyingi katika hlamashauri zote nchini zitashiriki.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya NMB, Edwin Mhede alisema kuwa Benki ya NMB
imeamua kuja na kampeni hii kwani ni Ajenda ya kidunia na taasis kama NMB
hawana Budi kuja na kampeni kama hii kwani ni jambo lenye manufaa kwa taifa.
Katika hafla hiyo, Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo alisema kuwa wata hakikisha wana shirikiana vyema na Benki ya NMB kwa kuwapatia mishe bora ya miti pamoja na utaalamu walionao katika masuala ya miti ili kuhakikisha kampeni ya miti milioni inatimia.
No comments:
Post a Comment