PROF. MBARAWA AKAGUA UJENZI WA SGR ISAKA-MWANZA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya

Thursday 19 January 2023

PROF. MBARAWA AKAGUA UJENZI WA SGR ISAKA-MWANZA

Eng. Christopher Kalist akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa alipokagua ujenzi wa reli ya kisasa  SGR sehemu ya Isaka-Mwanza KM 341, (kushoto), ni Mkurugenzi mkuu wa TRC Bw, Masanja Kadogosa.

Muonekano wa mataruma ya zege yakiwa katika hatua za utengenezwaji wake katika karakana ya Seke sehemu ya Isaka-Mwanza.

Muonekano wa reli ya SGR na treni ya ufundi ambayo ujenzi wake unaendelea sehemu ya Isaka-Mwanza.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa akiteta jambo na mkuu wa mkoa wa Mwanza  Bw, Adam Malima walipokagua jengo la abiria katika kiwanja cha ndege cha Mwanza.

WAZIRI wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa amezungumzia kuridhishwa kwake na kasi ya ujenzi wa reli ya kisasa SGR sehemu ya Isaka-Mwanza KM 341 na kuwataka wakazi wa kanda ya ziwa kujipanga kutumia fursa hiyo ya uchumi.

Amesema wakati ujenzi wa SGR ukiendelea ni wakati wa wadau mbalimbali kubuni fursa za kibiashara na kihuduma zitakazoendana na matumizi ya treni mpya ya kisasa.

“Fursa za reli ni nyingi hivyo hakikisheni mnaziibua ili kuwezesha huduma ya treni itakapoanza kufanyakazi kwa tija”, amesema Prof. Mbarawa.

Aidha amewataka wafanyakazi wa reli hiyo kuwa  wazalendo kwa kuepuka tabia za wizi kwani tabia hizo zinaweza kuchelewesha mradi na kuleta hasara kwa Serikali na Mkandarasi.

Amesema ujenzi wa barabara za lami, meli katika ziwa Victoria, reli ya kisasa (SGR) na uboreshaji wa uwanja wa ndege ni dhamira ya Serikali kuunganisha mikoa na nchi jirani kwa usafiri wa njia zote hivyo ni vema kwa watanzania kujivunia miradi hiyo.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Bw, Adam Malima amemshukuru Waziri Mbarawa kwa ufuatiliaji wa mara kwa mara wa miradi ya miundombinu mkoani humo na kumuahidi kuboresha huduma za ulinzi na usalama kwenye miradi hiyo ili ikamilike kwa wakati.

“Mheshimiwa Waziri sisi Mwanza tunajengewa daraja la Kigongo –Busisi, meli za kutoa huduma ukanda wote wa ziwa Victoria, jengo la abiria katika uwanja wa ndege na SGR ndio itapita juu hapa mjini hivyo tunafarijika sana kwa kweli”, amesema Mkuu wa mkoa Malima.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TRC Bw, Masanja Kadogosa amesema ujenzi wa sehemu ya tano ya SGR umefikia asilimia 23.4 na kumhakikishia Waziri Mbarawa kuwa wataendelea kumsimamia mkandarasi kikamilifu ili kazi ikamilike kwa wakati na ubora unaokusudiwa.

Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi.

No comments:

Post a Comment