TPA NA TRC YAANZA KUTEKELEZA MAELEKEZO YA MAKAMU WA RAIS BANDARI YA TANGA - THE HABARII

THE HABARII

HABARI | MATUKIO | MICHEZO.


ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday, 22 November 2022

TPA NA TRC YAANZA KUTEKELEZA MAELEKEZO YA MAKAMU WA RAIS BANDARI YA TANGA

 

Muonekano wa hatua iliyofikiwa ya ukarabati wa reli ya kutoka Stesheni ya Tanga kuelekea Bandarini, jijini Tanga. Ukarabati huo umeanza kufanyika  baada ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango kuelekeza Shirika la Reli Tanzania (TRC) na Mamlaka ya Bandari Nchini (TPA) kurejesha huduma za reli bandarini hapo.

Naibu Waziri wa Uchukuzi Atupele Mwakibete akiangalia miundombinu ya reli ya kutoka Stesheni ya Tanga kwenda Bandari ya Tanga, wakati alipokagua utekelezaji wa maelekezo ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ya kuikarabati reli hiyo na kurudisha vipande vilivyotolewa wakati alipokagua maendeleo ya mradi wa bandari ya Tanga.

No comments:

Post a Comment