Picha ya pamoja kati ya Waziri wa Miundombinu wa Burundi, Captain Dieudonne Dukundane na ujumbe wake pamoja na Menejimenti ya TANROADS mara baada ya mazungumzo yao. |
Picha ya pamoja kati ya Waziri wa Miundombinu wa Burundi, Captain Dieudonne Dukundane na ujumbe wake pamoja na Menejimenti ya TANROADS mara baada ya mazungumzo yao. |
Kikao kati ya Waziri wa Miundombinu wa Burundi, Captain Dieudonne Dukundane na ujumbe wake pamoja na Menejimenti ya TANROADS kikiendelea leo jijini Dar es Salaam. |
WAZIRI wa Miundombinu wa Burundi, Captain Dieudonne Dukundane amezungumzia umuhimu wa ushirikiano katika ujenzi wa barabara kati ya Tanzania na Burundi ili kurahisisha huduma ya usafiri na uchukuzi baina ya nchi hizo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam
leo alipotembelea Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mhe. Dukundane
ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa namna inavyojenga Barabara nzuri na nyingi
katika ushoroba wa Kati hali inayochochea maendeleo na kurahisisha huduma za
uchukuzi katika ukanda huo.
“…Tunawashukuru sana kwa kazi kubwa
ya ujenzi wa barabara nzuri, asilimia 80 ya magari ya Burundi yanayobeba mizigo
yanatumia barabara za Tanzania,” amesema Mhe. Dukundane.
Aidha amesema Burundi itatuma
wataalam wake wa masuala ya barabara kuja kujifunza TANROADS ili barabara za
Burundi zifanane na za Tanzania kwa ubora na usalama.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa
TANROADS, Eng. Rogatus Mativila ameahidi kutoa ushirikiano kwa taasisi ya
Ujenzi ya Burundi ili kuiwezesha kiutaalam na uwezo katika kufikia malengo yake
na ya nchi za ushoroba wa Kati kwa ujumla.
Eng. Mativila amebainisha kuwa
asilimia 90 ya mizigo inayoingia na kutoka Tanzania hutumia njia ya barabara
hivyo ushirikiano kati ya nchi hizo utaleta tija kwa pande zote katika sekta ya
usafiri na uchukuzi na hivyo kuchochea biashara na ujirani mwema.
Waziri Dukundane yuko nchini kwa ziara
ya kujifunza namna sekta za ujenzi na uchukuzi zinavyofanya kazi kwa pamoja
katika kuleta tija na ufanisi ambapo tayari ameshatembelea taasisi zilizochini
ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi za TPA, TRC na TANROADS.
No comments:
Post a Comment