WAFANYAKAZI BENKI YA NMB WAANZA KUPANDA MLIMA KILIMANJARO - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday, 10 October 2022

WAFANYAKAZI BENKI YA NMB WAANZA KUPANDA MLIMA KILIMANJARO

Msafara wa wafanyakazi wa NMB wanaopanda Mlima Kilimanjaro wakiwa katika picha ya pamoja na wenzao wa Matawi ya Moshi, waliofika kuwatakia kila la kheri kabla ya safari yao ya siku 7.

Msafara wa wafanyakazi wa NMB wanaopanda Mlima Kilimanjaro wakiwa wameanza safari yao ya siku 7.

Ofisa Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) – Charles Ng’endo, akiwakabidhi rasmi bendera wafanyakazi wa Benki ya NMB watakayoipeperusha katika kilele cha Mlima Kilimanjaro. Akishuhudia ni Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini-Dismas Prosper (Mwenye  tisheti ya bluu).

IKIWA ni mwendelezo wa kuadhimisha mwezi wa huduma kwa wateja, wafanyakazi 6 wa Benki ya NMB jana wameanza safari ya siku 7 ya kupanda Mlima Kilimanjaro kupitia geti la Machame ambapo wataipeperusha bendera ya benki hiyo katika kilele cha mlima huo.

Akizungumza katika hafla ya kuwaaga na kuwakabidhi rasmi bendera wafanyakazi hao, Ofisa Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA), Charles Ng’endo alisema kama Hifadhi ya KINAPA wamefarijika sana na utaratibu iliofanywa na NMB katika kuadhimisha mwezi huu muhimu wa huduma kwa wateja kwa kupanda Mlima Kilimanjaro, aidha wao kama hifadhi  watahakikishia kuwa wamewawekea mazingira mazuri na utaratibu mzuri wa kuwahudumia mpaka wanafika kileleni.

Aliongeza kuwa “kufanya hivi kunatusaidia kutangaza utalii wa ndani na tunafahamu hifadhi ya Taifa TANAPA na NMB tumekuwa na mahusiano ya karibu ya kibiashara na kiutoaji wa huduma kwa wananchi. Hivyo, kupanda Mlima Kilimanjaro na kufika kileleni kutaimarisha mahusiano kati yetu sote na kupeleka ujumbe kwa wateja wetu kuweza kutangaza utalii wa ndani,”

Naye Meneja wa benki hiyo Kanda ya Kaskazini-Dismas Prosper alisema kuwa, NMB kwa kutambua umuhimu wa sekta ya Utalii hapa nchini, waliona ni jambo la kifahari kusherekea mwezi wa huduma kwa wateja pamoja na wateja wao ambao wapo katika hii kwa kupandamlima Kilimanjaro ili kuutangaza mlima huo. Timu hiyo imepandishwa Mlima na kampuni ya Zara tours yenye uzoefu wa miaka mingi.

Akimalizia kuzungumza, kiongozi wa msafara huo wa wafanyakazi wa NMB ambaye pia ni Afisa Mkuu wa Wateja Wakubwa wa NMB – Alfred Shao alisema kuwa, NMB imefanya mambo mengi makubwa hapa nchini ikiwamo kuwa Benki bora na yenye masuluhisho mengi ya kifedha kwa wateja wao na kwamba wanataka kuwadhihirishia umma na wateja wao kuwa wanao uwezo wa kuwahudumia mpaka kilele cha Mlima Kilimanjaro na wajue wanamaanisha wanaposema ‘NMB Karibu Yako’.

Wengine waliopanda Mlima ni Nishad Jinah, Stella Motto, Reginald Baynit, Agnes Mlolele na Christopher Mwalugenge.

No comments:

Post a Comment