SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Zambia zinakutana jijini Lusaka, Zambia kujadili masuala ya ushirikiano yaliyokubaliwa baina ya nchi hizo mbili.
Majadiliano hayo yanafanyika katika Mkutano wa Kumi wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano - ngazi ya wataalam unaofanyika leo tarehe 11 Oktoba 2022. Mkutano huu utafuatiwa na mkutano ngazi ya Makatibu Wakuu utakaofanyika tarehe 12 Oktoba 2022 na mwisho utamalizika kwa mkutano ngazi ya Mawaziri utakaofanyika tarehe 14 Oktoba 2022 jijini Lusaka Zambia.
Mkutano huu unajadili na kutathimini utekelezaji wa maazimio katika sekta mbalimbali za ushirikiano zilizokubaliwa katika mkutano wa tisa uliofanyika tarehe 25 hadi 26 Februari 2016 jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Maeneo ya ushirikiano ni pamoja na; Siasa, Ulinzi na Usalama, Mambo ya Nje, Uhamiaji, Fedha na Uchumi, Sheria, Nishati, Habari na Mawasiliano, Kilimo, maendeleo ya miundombinu, Uchukuzi na Usafirishaji, Elimu, Sayansi na Teknolojia, Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Utalii, Kilimo, Uvuvi, Mazingira na Maliaasili, Afya, Elimu, Vijana na Michezo na jinsia.
Mkutano huu unafanyika kufuatia maagizo ya Marais wa pande zote mbili wakati wa ziara ya kiserikali ya Rais wa Jamhuri ya Zambia nchini Tanzania, Mhe. Hakainde Hichilema mapema mwezi Agosti 2022.
10th meeting of the Joint Permanent Commission (JPC) - Senior Officials Session is underway in Lusaka, Zambia. This preparatory meeting for the Permanent Secretary Meeting to held on 12 October 2022 is conducted under 3 clusters namely; Foreign Affairs, Defence & Security Cluster, Economic Cluster and Social Cluster.
Ambassador Hassan Yahya Simba leads the Tanzania delegation to the 10th meeting of the Joint Permanent Commission (JPC) - Senior Officials Session held in Lusaka Zambia. The meeting will be followed other sessions namely; Permanent Secretary Sessions on 12 October 2022 and Ministers Sessions to be held on 14 October 2022.
No comments:
Post a Comment