Katibu Mkuu wa TAMUFO, Stella Joel. |
Na Dotto Mwaibale, Arusha.
UMOJA wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO) umepongezwa kwa kuandaa kwa mara ya
pili Siku ya Muziki Duniani
(International Music Day 2022) hapa nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari Katibu Mkuu wa TAMUFO, Stellah Joel
alisema wamepokea pongezi nyingi kutoka kwa wadau wa muziki kuhusu maandalizi na maadhimisho ya siku hiyo.
Alisem maadhimisho ya siku hiyo yanafanyika kila mwaka ambapo wanamuziki
hapa nchini wanaungana na wenzao duniani kote kufurahia siku hiyo.
Alisem maadhimisho hayo yalianzishwa na Shirika la Umoja wa Mataifa
la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) miaka mingi iliyopita lakini kwa
Tanzania TAMUFO ndio waanzilishi na kuwa lengo lao likiwa ni kupanua wigo kwa
wanamuziki hapa nchini kuweza kuungana
na wenzao kimataifa na kuinua hadhi ya muziki duniani na Tanzania kwa ujumla.
Alisem maadhimisho hayo kila mwaka hufanyika Oktoba 1 na kuwa hapa nchini
yalianzishwa tangu mwaka 2021 na kitaifa yanafanyika jijini Arusha ambayo mwaka
huu yalifanyika katika Uwanja wa Makumbusho ya Elimu Viumbe kuanzia Septemba 28 hadi kilele chake
kilifanyika Oktoba 1, 2022, wilayani Karatu na kuhusisha wanamuziki wa kada zote.
Akizungumzia kwa nini maadhimisho hayo yanafanyika Arusha alisema sababu Arusha inaanza na herufi A na ni katikati ya Afrika na hata harakati nyingi za kudai uhuru zilifanyika Arusha na ndio maana na wao wakaona wafanyie hapo lakini.baadae wataweza kuadhimisha katika mikoa mingine.
Mlezi wa TAMUFO na mmoja aa waanzilishi wa Dk. Frank Richard alisema
wataendelea kuadhimisha siku hiyo kila
mwaka na akawaomba wadau wamaendeleo kutoa ushirikiano katika kuunga
mkono juhudi hizi ili kuleta Maendeleo katika Tasnia ya Muziki kwa ujumla
Dk. Richard aliishukuru Serikali, viongozi wa Mkoa, Wilaya, Taasisi, Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Cosota na Makumbusho ya Taifa kwa ushirikiano waliutoa na kuhakikisha maadhimisho hayo yanafanyinka vizuri huku pia akilishuru jeshi la polisi.
Mlezi wa maadhimisho haya hapa nchini, Toriano Salamba alisema watafanya maboresho makubwa katika maadhimisho haya kuhakikisha yanakuwa katika ubora wa kimataifa.
No comments:
Post a Comment