Na MJJWM- Dodoma
NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maaalum Wakili Amoni Mpanju, amesema jamii ya Kitanzania ili iweze kukuza uchumi wake lazima Vyuo vya Maendeleo ya Jamii nchini viwekeze zaidi kwa watu kwa kuwapatia maarifa yanayoendana na wakati wa sasa.
Wakili Mpanju amesema kuwa kupitia Ibara ya 229 ya Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya 2020 kwenda 2025 imeelekeza kuwapatia Vijana ellimu na juzi ili waweze kujikwamua na kujiinua kiuchumi.
Wakili Mpanju ametoa wito huo wakati akifunga Mkutano wa Mwaka wa Tathmini wa Viongozi wa Vyuo na Taasisi zilizopo chini ya Wizara hiyo uliofanyika kwa siku Sita jijini Dodoma kuanzia Oktoba 17 hadi 22, 2022.
Akifunga Mkutano huo Mpanju amevitaka Vyuo na Taasi hizo kuweka kipaumbele katika dhana tatu za uwanagenzi, Maarifa na Ushirikishwaji wa jamii sambamba na kufanya tafiti huku akiwasisitiza kuzingatia Sheria, taratibu na Miongozo kwa Miradi inayo tekelezwa.
“Mhakikishe hizi dhana tatu za uanagenzi ambazo ni ushirikishaji wa jamii, ubunifu na maarifa mnaweka mikakati madhubuti ili kuendeleza na kusimamia maeneo hayo” alisema Mpanju
Aidha Mpanju amevitaka Vyuo na Taassisi hizo kuongeza nguvu katika maeneo yenye changamoto ambayo ni eneo Utafiti na huduma shirikishi na kama tatizo ni Bajeti itengewe kwa mwaka wa fedha ujao wa fedha na pia ninyi wawe na ushirikiano na vyuo vya ndani na nje ya nchi.
Pia Naibu Katibu Mkuu Mpanju amewaagiza wakuu hao Vyuo, Waratibu na Wakufunzi wa Vyuo kuhakikisa wanapinga na kukemea ukatili unaojitokeza na unaoendelea kushamili katika jamii kwa kuanzisha madawa ya Jinsia ili yaweze kusaidiana kupambana na vitendo hivyo.
“Tuna janga la ukatili wa wanawake na watoto, kitu ambacho kinaathiri nguvu kazi ya taifa na kuondoa amani kwa familia na Jamii, hivyo mnatakiwa muanze kuandaa midahalo yenye lengo la kujadili changamoto za jamii,muweke ushirikiano na serikali za Mitaa ili kuleta mabadiliko” alisema Mpanju
Naibu Katibu Mkuu Mpanju ametumia pia fursa hiyo kuwaagiza wajumbe wa Mkutano huo kutoa kipaumbele kwenye suala la Utunzaji wa Mazingira kwa kuishirikisha Jamii inayozunguka Taasisi hizo sambamba na kuwataka Wanafunzi kupanda miti mitano mitano kila mmoja pindi anapojiunga na Chuo huku akiwataka kuweka mipaka ya Chuo na kuhakikisha wanapata hati miliki kwa ambao bado hawajafanya hivyo ili kuepusha migogoro na jamii.
Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi Usimamizi wa Vyuo kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Neema Ndoboka amesema lengo la kufanya mkutano huo ni kufanya tathmini ya mwaka kabla yakuanza kwa msimu Mpya wa Mwaka wa masomo ili waweze kuboresha utendaji kazi wa vyuo na kuleta matokeo change na tija iliyokusudiwa.
“Wizara imekua na taratibu ya kufanya tathmini kwa kuitisha vikao hivi kila mwaka kabla ya kuanza mwaka wa masomo ili kusaidia uendeshaji wa Vyuo vyetu vya Maendeleo ya Jamii kwa kubaini Changamoto na Kuweka maazimio yatakayoleta tija” alisema Ndoboka.
No comments:
Post a Comment