Na Mwandishi Wetu, Pwani
Akizungumza jana wakati wa tukio la upokeaji wa vifaa vya ujenzi (matofali na nondo) vilivyotolewa na wanafunzi waliosoma shule hiyo tangu ilipoanzishwa mwaka 1977 mpaka sasa,
Mkuu wa Shule ya Ruvu Sekondari Juliana Chimanzi alisema uzio wa shule ni muhimu kwani kuna changamoto ya mifugo kuingia eneo la shule lakini pia wezi na vibaka.
"Nitoe Serikali, wadau na kwa namna ya kipekee wanafunzi waliopita hapa kokote waliko watusaidie.Shule yetu ina idadi kubwa wanafunzi wasichana ambao wanafikia 850 , tunahitaji kuweka ulinzi kwa kujengewa uzio.Tumefanya tathimini Sh.Sh.milioni 794.9 zinahitajika,”aamesema.
Awali akizungumza baada ya kukabidhi vifaa hivyo vya ujenzi, Mwenyekiti wa Wanafunzi waliosoma kwenye shule hiyo kwa nyakati tofauti Veronica Chambuso kuanzia mwaka 1977 amesema wameona wachangishane ili peleka vifaa vitakavyosaidia kuanza ujenzi wa uzio.
“Tumeleta matofali na nondo , huu ni mwanzo lakini tunaendelea kuwaomba waliosoma Ruvu Sekondari kuanzia mwaka 1977 mpaka sasa na miaka inayokuja, wazazi , wafadhili na wale wanaoguswa na ulinzi wa watoto wa kike tushirikiane kwani ukimlinda mtoto wa kikekwani akapata elimu itamsaidia na taifa litanufaika,”alisema Chambuso.
Amefafanua kwamba shule hiyo ilijengwa mwaka 1977 baada ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere kuomba msaada Serikali ya Cuba, hivyo wanamshukuru kwa upendo wake na katika kumuenzi wameona kuna uhitaji mkubwa wa uzio.
Kwa upande wao Waratibu wa Uchangiaji huo ambao nao ni sehemu ya wanafunzi waliosoma shule hiyo Devota Makililo na Victoris Massawe wameendelea kuhamasisha wadau kuendelea kuchangia ujenzi huo.
“Tunaomba wadau na Wizara ya Elimu kuona huruma kwa shule ya wasichana watusaidie kwenye kujenge uzio.Pia kwa unyenyekevu mkubwa tunamuomba Rais Samia Suluhu Hassan atusaidie kufanikisha ujenzi huu.Watoto kike wakihitaji kuangaliwa na amekuwa akilisemea hilo mara kwa mara,”ameongeza.
Wakati huo huo Dada Mkuu wa Shule ya Sekondari Ruvu Jacquline Mgisha anayesoma kidato cha Sita alisema wanashukuru wanafunzi waliopita shuleni hapo kutambua umuhimu wa jambo hilo.
“Uzio ni muhimu sana kwetu , hivi makazi ya watu yamekuwa karibu na shule na hivyo kuhatarisha usalama wa wanafunzi.Pia tunamuomba mama yetu Rais Samia Samia Suluhu kutusaidia na hatimaye tuwe na uzio na sisi tutamlipa kwa kufanya vizuri kwenye masomo,”amesema.
No comments:
Post a Comment