Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Emmanuel Tutuba (kushoto) na Balozi wa Serikali ya Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani nchini Tanzania Regine Hess (kushoto) wakitia saini ya mkataba wa msaada Euro Mill 10 kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi mitatu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Emmanuel Tutuba (kushoto) na Balozi wa Serikali ya Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani nchini Tanzania Regine Hess (kushoto) wakibadilishana mikataba waliosaini kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi mitatu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Emmanuel Tutuba akizungumza baada utiaji wa saini ya mkataba wa msaada Euro Mill 10 kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi mitatu.
Balozi wa Serikali ya Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani nchini Tanzania Regine Hess akizungumza baada utiaji wa saini ya mkataba wa msaada Euro Mill 10 kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi mitatu.
Picha ya pamoja (Na Mussa Khalid).
NA
MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
SERIKALI ya Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani imeipatia serikali ya Tanzania msaada wa Jumla ya Euro Mill 10 sawa na Shilingi za
Kitanzania Bill 23.7 kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi mitatu.
Hayo
yamejiri leo jijini Dar es salaam katika Hafla ya utiaji wa saini wa mkataba wa
ushirikiano kati ya serikali hizo mbili kuhusu miradi mitatu ukiwemo mradi Euro
Mill 6 kwa ajili ya kukabiliana na migogoro au muingiliano kati ya wanyama na binadamu kwenye maeneo
yanayozunguka hifadhi.
Akizungumza
katika hafla hiyo ya utiaji wa saini,Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango
Emmanuel Tutuba amesema miradi mingine ni mradi wa Euro Mill 3 kwa ajili ya
kuwezesha upatikanaji wa haki za wanawake na watoto na wa Euro Mill 1 kwa lengo
la kuandaa maandiko ya kitaalamu na kufanya tafiti.
Aidha
Tutuba amesema mradi wa kuwezesha upatikanaji wa haki za wanawake na watoto
utawezesha makundi maalum kwa kuwa na uwezo wa kudai haki zao na hivyo
kupunguza unyanyasaji wa Kijinsia katika maeneo ya utekelezaji wa miradi hiyo.
‘Kuhusu
fedha za mradi wa kuandaa maandiko ya
kitaalamu na kufanya tafiti zitawezesha kufanya pembuzi yakinifu kwa miradi
mbalimbali itakayoiwezesha serikali kupata misaada kwa siku za usoni kupitia
Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani’amesema Tutuba
Kwa
upande wake Balozi wa Serikali ya Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani nchini
Tanzania Regine Hess amesema wataendelea kushirikiana na Tanzania katika
kusaidia kufanikisha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimaendeleo.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Khatibu Kazungu ameipongeza serikali
ya Ujerumani kwa msaada huo kwani utakwenda kusaidia kupunguza kesi za ukatili
wa kijinsia kwa kina mama wazee na watoto nchini.
Naye
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Juma Mkomi amesema msaada huo
umekuja muda muafaka kwani utasaidia kukabiliana na changamoto zinazojitokeza
baina ya binadamu na wanyama huku pia akiwataka wananchi kuepuka kuingia katika
maeneo yaliyohifadhiwa.
Hata hivyo Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Emmanuel Tutuba amemuhakikishia Balozi wa Ujerumani kuwa serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan itaendelea kutekeleza miradi hiyo na fedha zote kuelekezwa katika maeneo yaliyokusudiwa.

No comments:
Post a Comment