WAZIRI UMMY AZINDUA MITAMBO YA HEWA TIBA YA OKSIJENI YENYE THAMANI YA BILIONI 1.5 - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Saturday, 2 July 2022

WAZIRI UMMY AZINDUA MITAMBO YA HEWA TIBA YA OKSIJENI YENYE THAMANI YA BILIONI 1.5

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akizindua mitambo ya  kuzalisha hewa tiba ya Oksjeni  iliyogharimu bilioni 1.5 ambapo  zimetumika kununua mitambo, gari ya kusambazia mitungi ya oksijeni, mitungi 560  pamoja na ujenzi wa jengo ambalo mitambo hiyo imefungwa.

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akizindua kitabu cha mwongozo wa utoaji dawa (Benjamin Mkapa Hospital Formulary ) utakaotumiwa na waandika dawa (Prescribes), wafamasia, wachunguzi na wauguzi.


Na Catherine Sungura, WAF-Dodoma

WAZIRI  wa Afya Ummy Mwalimu amezindua mitambo wa hewa tiba ya Oksijeni wenye thamani ya bilioni 1.5 kwenye hospitali ya Benjamnin Mkapa iliyoko jijini Dodoma.

Waziri Ummy amesema usimikaji wa mitambo hiyo ni sehemu ya mikakati ya Serikali ya Awamu ya Sita katika kuhakikisha kuwa huduma zinaboreshwa na kuongeza kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja mitambo 14 imeshasimikwa kwenye hospitali za rufaa za mikoa nchini.

"Sisi kama Sekta tumejiwekea vipaumbele vyetu ambavyo Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan ingependa kuviona tunavitekeleza, kipaumbele kikubwa  ni ubora wa huduma za afya, hivyo mitambo hii ina lengo la kuokoa maisha kwa wananchi wake".

Waziri Ummy amesema wanatarajia kusimika mitambo mingine  57 ya hewa tiba ya Oksijeni kwenye hospitali za rufaa za mikoa,Kanda pamoja na Wilaya nchini.

Aidha, Waziri Ummy ameipongeza hospitali hiyo pamoja na Mkurugenzi Mtendaji Dkt.Alphonce Chandika  kwa kuhakikisha kuwa kazi ya usimikaji wa mitambo huo unakamilika kwa wakati  na unazingatia viwango vinavyotakiwa

Ameongeza kuwa mitambo hiyo haitosaidia hospitali hiyo tu bali hata hospitali na vituo vya mikoa wa Dodoma na mikoa ya jirani ikiwemo Manyara, Singid na Iringa.

Pia amesema licha ya mitambo  huo  ambao ni mradi mmoja kati ya miradi 17 ambayo inatekelezwa na Rais Samia Suluhu Hassan ambapo jumla  ya takribani Bilioni 10.02 zimeelekezwa katika kukamilisha miradi hiyo hospitalini hapo.

Naye,Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo Dkt. Alphonce Chandika amesema mitambo hiyo inazalisha mitungi 400 kwa siku na una sehemu mbili ambazo hazitegemeana hivyo unaweza kuwasha sehemu moja kipindi unatumia ili kuhakikisha uzalishaji unaendelea wakati wote hata wakati wa matengenezo kinga inapolazimu kuzima upande mmoja.

Dkt.Chandika aliongeza kabla ya hapo hospitali ilikua ikitumia mitungi 200 kwa mwezi  lakini kipindi cha UVIKO-19  matumizi yakiongezeka  hadi kutumia mitungi 200 kwa siku  na hivyo kuongeza gharama za uendeshaji wa hospitali na kutumia  milioni 10 kwa siku badala ya milioni 10 kwa mwezi kwa kipindi hicho cha UVIKO-19.

No comments:

Post a Comment