TAMASHA LA UTAMADUNI LAENDELEA KUWAPA FURAHA WATANZANIA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Sunday, 3 July 2022

TAMASHA LA UTAMADUNI LAENDELEA KUWAPA FURAHA WATANZANIA

Naibu Katibu Mkuu Saidi Yakubu.


Na Shamimu Nyaki - WUSM

TAMASHA la kwanza la Kitaifa la Utamaduni lililofanyika Julai 01 hadi 03, Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam limewapa furaha Watanzania ambao wamelifuatilia katika viunga vya jiji la Dar es Salaam na waliofuatilia kupitia Mitandao ya Kijamii na Vyombo vya Habari.

Akizungumza wakati anatoa neno la Utangulizi katika hafla ya kufunga Tamasha hilo, Naibu Katibu Mkuu Saidi Yakubu amesema kuwa, Tamasha hilo limeandika historia kwa nchi na wa miaka ijayo litaboreshwa zaidi.

"Tumewapa furaha Watanzania kama dhamira ya Wizara yetu, tumefanikiwa kuisimamisha Dar es Salaam na Tanzania kwa  ujumla na wananchi wameona Utamaduni wao na naamini wataendelea kuuenzi" amesisitiza Bw. Yakubu.

Ameongeza kuwa, dhamira ya Wizara ni kulifanya Tamasha hilo kuwa la Kimataifa na kufikia viwango vya matamasha ya Kitamaduni yanayofanyika duniani ikiwemo la nchini  Bzarili, Marekani na Uingereza.

Bw. Yakubu amesisitiza kuwa,  lengo la Tamasha hilo ni kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika kutangaza nchi yetu kupitia Utamaduni.

Ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa leo Julai 03, kutakua na  Usiku wa Taarabu na kukaribisha vikundi vyote vya ngoma vilivyoshiriki Tamasha hilo kuhudhuria Usiku huo ambao utapambwa na Wasanii Nguli wa Muziki huo, Vikundi kutoka Zanzibar na Tanga, pia kutakua na Vikundi kutoka nje ya nchi ikiwemo  Burundi, Kenya na Comorro.

No comments:

Post a Comment