Na Dotto Mwaibale, Singida
WANANCHI Mkoa wa Singida wamehimizwa kujitokeza kwa wingi kushiriki zoezi la
Sensa ya Watu na Makazi litaklofanyika Agosti 23, 2022.
Ombe hilo limetolewa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa (NEC) Mkoa wa Singida, Yohana Msita wakati akirudisha fomu ya kugombea nafasi
hiyo kwa kipindi kingine tena katika mchakato wa kupokea na kurudisha fomu kwa
wanachama wa chama hicho ulioanza jana.
"Nitumie nafasi hii kuwaomba wananchi wote mkoani hapa kujitokeza kwa
wingi kushiriki zoezi la sensa ya watu na makazi na kutoa ushirikiano kwa
maofisa watakuwa kuwa wakifanya kazi hiyo" alisema Msita.
Akizungumzia Umuhimu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 Msita alisema
ni pamoja na kuisadia Serikali kupata
taarifa za msingi zitakazosaidia mchakato wa utekelezaji wa Dira ya Maendeleo
ya mwaka 2025, mageuzi ya masuala ya afya na jamii, pamoja na ufuatiliaji wa
ajenda za maendeleo za kimataifa.
Alisema taarifa za idadi ya watu husaidia katika mamlaka za wilaya juu ya utekelezaji wa mipango ya maendeleo ambayo huakisi matakwa ya watu katika ngazi
husika na kusaidia kwenye uwiano wa mgawanyo wa rasilimali na kupata taarifa za
msingi za hali ya kidemografia, kijamii na kiuchumi za idadi ya watu na makazi
za mipango kwenye ngazi zote.
Aidha Msita alisema umuhimu wa sensa hiyo ni pamoja na kigawio katika
kukokotoa viashiria vingine mfano Pato la mtu mmoja mmoja, Pato la Taifa, Ajira
na ukosefu wa Ajira na kiwango cha uandikishaji wa wanafunzi.
Pia alisema umuhimu wa sensa hiyo ni kupata taarifa itakayowezesha serikali
kujua ongezeko la idadi ya watu, kwa mgawanyo na viashiria vingine, ambavyo ni
muhimu kwa usimamizi wa mazingira na msingi wa utawala bora na ujumuishaji wa
demokrasia.
Alisema Takwimu sahihi za Sensa zinahitajika kwa ajili ya ugawaji wa
majimbo ya uchaguzi kwa ufanisi, kurekebisha mipaka ya kiutawala katika
serikali za mitaa na maeneo mengine.
Msita alitumia nafasi hiyo kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi ambazo zimetekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani hapa ambapo kwa mwaka mmoja tangu awe madarakani mkoa wa Singida ulipatiwa Sh.230 Bilioni.
No comments:
Post a Comment