RAIS WA KAMATI YA OLIMPIKI TANZANIA GULLAM ABDULLAH RASHID NA KATIBU WAKE FILBERT BAYI WATEMBELEA KAMBI YA WANAMICHEZO WA TANZANIA MASHINDANO YA JUMUIYA YA MADOLA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday, 26 July 2022

RAIS WA KAMATI YA OLIMPIKI TANZANIA GULLAM ABDULLAH RASHID NA KATIBU WAKE FILBERT BAYI WATEMBELEA KAMBI YA WANAMICHEZO WA TANZANIA MASHINDANO YA JUMUIYA YA MADOLA

Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) Filbert Bayi akiongea na wanamichezo wa Tanzania watakaoshiriki kwenye Michezo ya Jumuiya ya Madola wakati yeye na Rais wa TOC Gullam Abdullah Rashid (wa pili kulia) walipowatembelea katika kijiji cha wanamichezo kilicho katika Chuo Kikuu cha Birmingham, Uingereza, ambako mashindano hayo yanafunguliwa rasmi siku ya Alhamisi Julai 28, 2022. Wengine pichani ni Makamu wa Rais wa TOC Henry Tandau na Meneja wa timu Suleiman Jabir Mahmoud.

Rais Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) Bw. Gullam Abdullah Rashid (walioketi wa pili kulia) na Katibu Mkuu wake Bw. Filbert Bayi wakiongea na  wanamichezo wa Tanzania watakaoshiriki kwenye Michezo ya Jumuiya ya Madola na viongozi wao walipowatembelea kuwajulia hali na kuwatia moyo kambini kwao katika kijiji cha wanamichezo kilicho katika Chuo Kikuu cha Birmingham, Uingereza, ambako mashindano hayo yatayofunguliwa rasmi siku ya Alhamisi Julai 28, 2022 yanaandaliwa. Wengine walioketi nao ni Makamu wa Rais wa TOC Bw. Henry Tandau (wa pili kushoto) na Meneja wa timu Suleiman Jabir Mahmoud (kushoto).

No comments:

Post a Comment