Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa Benki ya NBC, Godwin Semunyu(wa kwanza kushoto) na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa NBC, David Raymond wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa zawadi watakazokabidhiwa washindi wa mbio za Kimataifa za NBC Dodoma international Marathon 2022.Kulia ni mtangazaji wa kipindi cha Joto la asubuhi, Gerland Hando pamoja na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa EFM, Denis Busulwa.Benki hiyo imetangaza kutoa jumla ya Sh65 milioni kwa washindi wa mbio hizo zitakazofanyia Julia 31,2020 mkoani Dodoma.
Dar es Salaam. Haijawahi kutokea! ndivyo unavyoweza kuzielezea zawadi zitakazotolewa kwa washindi wa mbio za NBC Dodoma International Marathon ambapo jumla ya Sh65 milioni zitagawiwa kwa washindi 15 watakaoibuka kidedea kwenye mbio hizo. Mbio hizo za Kimataifa zitakayofanyika siku ya Jumapili, Julai 31,2022 mkoani Dodoma na zitahusisha Kilomita 42, Kilomita 21 na kilomita 10 huku dhumuni likiwa ni kuchangia mapambano dhidi ya ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi.
Akitangaza zawadi za washindi, Kaimu Mkuu wa kitengo cha masoko wa NBC, David Raymond alisema maandalizi yamekamilika na kwamba zawadi zitakazotolewa zimelenga kutoa hamasa kwa wakimbiaji hasa wa ndani.
Mshindi wa kwanza katika mbio za Kilomita 42 kwa upande wa Wanaume na Wanawake ataondoka na kitita cha Sh8, 000,000 kila mmoja huku wa pili akijitwalia Sh4, 000,000 wa tatu Sh2, 000,000 wa nne Sh1,500,000 huku wa tano akijitwalia Sh1,000,000.
“Kwa kuzingatia kuwa mcheza kwao hutunzwa, kwa mtanzania ambaye atakuwa wa kwanza ‘Overall Winner’ atapata Shilingi milioni nane na ataongezewa Shilingi milioni 2 kwahiyo ataondoka na jumla ya Shilingi milioni 10,” alisema.
Kwa upande wa Kilomita 21, mshindi wa kwanza atapata Shilingi milioni nne ambapo mtanzania atakayeshika nafasi hiyo kuongezewa Shilingi Milioni moja na kufanya jumla ya Shilingi 5,000,000.
Mshindi wa pili atapata Sh2, 000,000, wa tatu 1,500,000 wa nne 1,000,000 wakati wa tano atajitwalia Sh. 700,000.
Mbio za Kilomita 10 mshindi atajipatia Sh. 1,500,000 wa pili Sh. 1,000,000 wa tatu Sh. 700.000 wa nne Sh. 500,000 wakati wa tano atajishindia Sh. 300,000.
Mkuu wa Kitengo Uhusiano wa NBC, Godwin Semunyu alisema mbio za mwaka huu zimelenga katika kutoa elimu ya saratani ambapo wameshirikiana na taasisi ya Ocean Road ili kufanikisha zoezi hilo.
“Kikubwa kwenye zoezi hili ni kutengeneza utamaduni wa kupima mara kwa mara na sisi tunaamini kwa kutumia Marathon hii itatupa platform(jukwaa) kubwa zaidi na tunaamini tutawafikia watu wengi zaidi,” alisema.
Aliongeza kuwa mbio hizo zitasaidia katika kufungua mipaka ya kibiashara katika mambo mbalimbali ikiwamo zao la zabibu ambapo wawekezaji watapata fursa ya kujionea uzalishaji wake na namna gani wanavyoweza kushikrikiana na Serikali kwenye eneo hilo.
Ili kujisajili kushiriki kwenye mbio hizi za kimataifa, unaweza kutembelea tovuti ya events.nbc.co.tz na kulipia ada ya Sh30,000 kwa mbio zote ambapo utajipatia vifaa vya kukimbilia ikiwamo jezi.
Mwisho//
No comments:
Post a Comment