Mwakilishi wa Mkurugenzi wa HLI kutoka Kenya, Bw. Kakieto Richard katika majadiliano na Padri Jonathan Opio Mkurugenzi wa HLI kutoka Uganda. |
Mkurugenzi wa HLI Kanda ya Afrika kwa nchi zinazozungumza lugha ya Kiingereza, Bw. Emily Hagamu akijadili jambo na Mwakilishi wa HLI kutoka Kenya, Bw. Kakieto Richard. |
Na Frida Manga
SHIRIKA la Kimataifa la Kutetea Uhai, Tawi la Afrika Mshariki (HLI), limewasilisha Barua Ofisi ya Bunge la Afrika Mshariki ya Kutaka kuonana na Sipika wa Bunge na kueleza mawazo yao juu changamoto zilizopo kwenye Muswada wa Ujinsia na Afya ya Kizazi Jumuiya ya Afrika Mashariki wa mwaka 2020/2021.
Barua hiyo iliwasilishwa Mei 23 mwaka huu na Viongozi wa (HLI) kwenye ofisi za Bunge la Afrika Mshariki zilizopo jijini Arusha.
Viongozi waliowasilisha ni pamoja na Emily Hagamu Mkurugenzi wa HLI Kanda ya Afrika kwa nchi zinzozungumza lugha ya Kingereza pia Mkurugenzi wa HLI Tanzania, Padri Jonathan Opio Mkurugenzi wa HLI Uganda, Kakieto Richard mwakilishi wa Mkurugenzi wa HLI Kenya na Aloys Ndengeye Mkurugenzi wa HLI Rwanda.
Kwa mujibu HLI, muswada huo unavipengele vinne ambavyo vinapingana na Utu, utashi, imani na mila na desituri za watu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Miongoni mwa vipengele hivyo ambavyo HLI wanasema ni viovu ni, kipengele kinachotaka ama kinacholazimisha Nchi za Afrika Mashariki kufanya matumizi ya vidhibiti mimba kuwa sehemu ya maisha yao bila kujali umri, wala hali ya ndoa na hasa kulazimisha matumizi yake kwa Watoto.
Pia kipengele kinachotaka Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kutunga Sheria za kutoa mimba, kulazimisha masomo ya ngono ambayo yanaharibu ukuwaji wa watoto na kuleta mmomonyoko wa maadili na Kuingilia kati uumbaji wa binadamu kwa kuhamasisha matumizi ya Tekenolojia Ili kupata uzao.
Mkurugenzi wa HLI Kanda ya Afrika kwa Nchi zinzozungumza Lugha ya Kingereza, Emeli Hagamu anasema (HLI) inataka Muswada huo ufanyaiwe marekebisho Ili uakisi maisha halisi ya kiuchumi, kijamii na Kimaadili ya watu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki pia utambue tunu za Kiimani na za Watu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
No comments:
Post a Comment