SHAKA AAGIZA WAKULIMA WA KOROSHO KUPATIWA PEMBEJEO HARAKA MKOA WA MTWARA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday, 3 June 2022

SHAKA AAGIZA WAKULIMA WA KOROSHO KUPATIWA PEMBEJEO HARAKA MKOA WA MTWARA

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Shaka Hamdu Shaka, akizungumza na mmoja wa wananchi waliojitikeza wakati akikagua mradi wa maji Maratani, Kata ya Maratani Wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara.



Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Shaka Hamdu Shaka, akizungumza baada kukagua Zahanati ya Namatumbusi katika Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara. (Picha zote na Fahad Siraji wa CCM).

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Shaka Hamdu Shaka, akicheza muziki pamoja na Kinana alipowasili katika Kijiji Cha Namatumbuasi  Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu, mkoani Mtwara akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka ameiagiza Serikali ya Mkoa wa Mtwara kuacha urasimu kwa kuchelewesha ugawaji wa pembejeo kwa wakulima wa korosho  mkoa humo.

Shaka ametoa maagizo hayo baada ya kuwasili Mkoa wa Mtwara kwa ziara ya kikazi akitokea mkoani Lindi ambapo baada ya kufika Mtwara alipata nafasi ya kusikiliza kero za wananchi na miongoni mwa kero hizo ni baadhi ya vijiji kutopata pembejeo hali inayotia wasiwasi kwamba huenda itachelewesha maandalizi mikorosho kuelekea msimu mpya wa zao hilo.

"Tumetoka asubuhi tumezungumza na Mkuu wa Mkoa taarifa ambayo nimepatiwa pembejeo zimeshafika, hivyo niwatake Serikali ya Mkoa wa Mtwara waache urasimu, ndani ya wiki moja pembejeo ziwe zimetoka, tunataka wananchi wanufaike na uwepo wa Rais Samia ambaye ameamua kutoa bure pembejeo za kilimo, lengo kuhakikisha wakulima wananufaika na kilimo chao," alisema Shaka.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Meja Jenerali Marko Gaguti, amesema  amepokea maelekezo hayo na atakwenda kuyafanyia kazi huku akiahidi pembejeo hizo kuanza kuwanywa leo hii wilayani humo.

No comments:

Post a Comment