NAIBU WAZIRI UJENZI NA UCHUKUZI, MHE. MWAKIBETE AFANYA ZIARA TMA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday, 28 January 2022

NAIBU WAZIRI UJENZI NA UCHUKUZI, MHE. MWAKIBETE AFANYA ZIARA TMA

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhe. Atupele Fredy Mwakibete (katikati) akizungumza na viongozi na wafanyakazi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) mara baada ya ziara yake kuangalia utendaji kazi wa TMA. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dkt. Buruhani Nyenzi pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) Dkt. Agnes Kijazi (kulia).

Mkurugenzi wa Utafiti na Matumizi ya Hali ya Hewa, Dk. Ladislaus Chang'a akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhe. Atupele Fredy Mwakibete (wa pili kushoto) namna idara ya kumbukumbu ya TMA inavyofanya kazi zake.


Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Agnes Kijazi (kulia) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhe. Atupele Fredy Mwakibete (wa pili kushoto) katika moja ya idara za TMA zinavyochakata utabiri kabla ya kuutawanya kwa wananchi kwa matumizi.


Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhe. Atupele Fredy Mwakibete (MB) akitoa maelekezo kwa menejimenti na wafanyakazi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) mara baada ya ziara yake, ambapo alifurahishwa na utendaji kazi wa TMA pamoja na ushirikiano wanaouonesha katika majukumu yao.

Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dkt. Buruhani Nyenzi akizungumza kumkaribisha Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhe. Atupele Fredy Mwakibete (MB) katika ziara yake ndni ya taasisi hiyo.

Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Agnes Kijazi (kulia) akitoa taarifa fupi kwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhe. Atupele Fredy Mwakibete (MB) kabla ya Naibu Waziri kuanza ziara yake kutembelea idara anuai za TMA kuangalia zinavyochakata utabiri kabla ya kuutawanya kwa wananchi kwa matumizi.

Sehemu ya viongozi na wafanyakazi wa TMA wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhe. Atupele Fredy Mwakibete (MB) akitoa maelekezo ya wizara mara baada ya ziara yake.

Sehemu ya viongozi na wafanyakazi wa TMA wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhe. Atupele Fredy Mwakibete (MB) akitoa maelekezo ya wizara mara baada ya ziara yake.


Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhe. Atupele Fredy Mwakibete (katikati) akipata maelezo kutoka kwa wataalam wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) alipofanya ziara yake kuangalia utendaji kazi wa TMA. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dkt. Buruhani Nyenzi.



Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhe. Atupele Fredy Mwakibete (katikati) akipata maelezo kutoka kwa wataalam wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) alipofanya ziara yake kuangalia utendaji kazi wa TMA. 

Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dkt. Buruhani Nyenzi (kushoto).
 akizungumza.

Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Agnes Kijazi (kulia) akizungumza.



No comments:

Post a Comment