Timu ya Taifa ya Tanzania ya Soka kwa Wenye Ulemavu (Tembo Warriors), ikipambana na timu ya Taifa ya Sierra Leone. |
Timu ya Taifa ya Tanzania ya Soka kwa Wenye Ulemavu (Tembo Warriors), ikipambana na timu ya Taifa ya Sierra Leone. |
TIMU ya Taifa ya Tanzania ya Soka kwa Wenye Ulemavu (Tembo Warriors), imeipa hadhi nchi kwa kuwa Taifa la kwanza Afrika, kufuzu kwenda Robo Fainali za Mashindano ya Soka kwa Walemavu Afrika (Canaf), ambayo Tanzania ni mwenyeji.
Tanzania imepata nafasi hiyo baada ya leo kuifunga timu ngumu ya Taifa ya Sierra Leone bao 1-0 kwenye mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam.
“Sasa tuna mechi moja mbele kabla ya kupata tiketi mbili muhimu; moja ni kuingia nusu fainali lakini tukishinda mechi hiyo moja pia tutakuwa tumefuzu moja kwa moja kwenda Kombe la Dunia litakalofanyika mwakani mjini Instanbul, Uturuki,” alisema Katibu Mkuu wa Wizara ya Michezo Tanzania, Dkt. Hassan Abbasi akizungumza na wachezaji hao baada ya mechi.
No comments:
Post a Comment