SHIRIKA LA MEDO LAWEZESHA SIKU YA MTOTO WA KIKE DUNIANI, SINGIDA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday, 12 October 2021

SHIRIKA LA MEDO LAWEZESHA SIKU YA MTOTO WA KIKE DUNIANI, SINGIDA

Wanafunzi wakitoa burudani kwenye maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike Duniani yaliyofanyika Ilongero Wilaya ya  Singida mkoani Singida jana.

Wanafunzi wakiwa katika matembezi ya kuadhimisha siku yao wakiwa na mabango yaenye ujumbe mbalimbali.

Mkuu wa wilaya hiyo Mhandisi Padkas Muragili ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo akihutubia.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida Esther Chaula akizungumza kwenye maadhimisho hayo.

Wanafunzi wakiwa kwenye maadhimisho hayo.

Mratibu wa Shirika lisilokuwa la Kiserikali la MEDO, Idd Hashim, akizungumza  kwenye maadhimisho hayo.

Wakina mama wakitoa burudani kwenye maadhimisho hayo.

Mwakilishi wa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini akitoa salamu za Mbunge kwenye hafla hiyo.

Wazazi na walezi wakiwa kwenye hafla hiyo.

Diwani wa Viti Maalumu wa Kata hiyo Mhe. Mosha akitoa neno la shukurani katika Maadhimisho hayo.

Mgeni rasmi katika picha ya pamoja na wanafunzi.

Mgeni rasmi katika picha ya pamoja na wanafunzi.

Mgeni rasmi katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Shirika la MEDO.

Risala kutoka Shirika la MEDO ikisomwa.


 Msichana Sheila Nyalandu Kijana wa Kata ya Ilongero aliyekatishwa masomo na bodaboda kwa kupewa ujauzito akitoa ushuhuda wa mambo kadhaa yaliyo mshawishi hadi akapata ujauzito.

Boniphace Jilili na Dotto Mwaibale, Singida

WAZAZI/Walezi wametakiwa kuwatafutia njia mbadala watoto wao wa kike ya kujikwamua kiuchumi inapotokea kukatishwa ndoto zao kwa kushindwa kuendelea na masomo kwasababu mbalimbali ikiwemo kubebeshwa mimba.

Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskas Muragili alitoa wito huo jana wakati alipokuwa akizungumza kwenye hafla ya kilele cha maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani yaliyofanyika kiwilaya katika mji mdogo wa Ilongero wilayani Singida.

Muragili alisema siku hiyo inapaswa kuchukuliwa kwa umuhimu wake kwani inaenda kuleta mapinduzi makubwa ya kumkomboa mtoto wa kike kutokana na wazazi kupata uelewa juu ya haki za mtoto.

"Jamii zetu huko nyuma hazikuwa zinawapa fursa mtoto wa kike hasa haki ya kupata Elimu,lakini baada ya kuanzishwa siku hii kwa mara ya kwanza mwaka 2012 imesaidia kwa kiasi kikubwa na tumeona mtoto wa kike akishika nafasi mbalimbali za kiuongozi." alisema Muragili.

Aliwaambia mapambano ya kumkomboa mtoto wa kike hayawezi kufanikiwa kama wazazi hawatashiriki kikamilifu katika mapambano hayo kwa kuwafichua wanautekeleza vitendo vya ukatili,hivyo amewaomba wazazi kushiriki kikamilifu.

"Halafu Wazazi tujitahidi sana kuwatimizia watoto wetu hasa watoto wa kike mahitaji yao ili wajiepushe kuingia kwenye tamaa zitakazo wapelekea kushindwa kufikia malengo yao." alisema Muragili.

Awali Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Esther Chaula aliwataka Wazazi kujitahidi kugawa majukumu sawa yatakayompa nafasi mtoto wa kike ya kupata mahitaji mengine kama fursa ya Elimu kwani licha ya Serikali kutoa Elimu bure bado kumekuwa na changamoto ya Wazazi kukandamizwa kwa kupewa majukumu mengi ya kufanya huko kwenye familia.

"Wazazi tuwe karibu na watoto wetu na hii itatusaidia kuona mapema mabadiliko ya watoto wetu na kuyadhibiti mapema kabla yayajaleta madhara." alisema Chaula.

Shirika la Maendeleo ya Elimu Mtinko (MEDO) lililopo mkoani hapa ndio limewezesha shughuli ya maadhimisho hayo yakienda sambamba na kauli mbiu yake "Kizazi cha kidijitali, Kizazi chetu"

Shirika hilo linatekeleza Mradi wa 'haki kodi'  kitaifa unatekelezwa na Serikali ya Norway kupitia ActionAid wenye lengo la kuondoa vikwazo na kuimarisha huduma zinazozingatia jinsia.

Akisoma risala mbele ya mgeni rasmi muhamasishaji kutoka Shirika hilo Emineema Peter alisema maadhimisho hayo yanalenga kuzitambua haki za mtoto wa kike na changamoto anazozipitia katika jamii ili ziweze kupatiwa ufumbuzi.

Alisema wakati wa janga la COVID-19 limeharakisha majukwaa ya kidijitali ya kujifunzia,kupata na kuunganisha watu.watu bilioni 2.2 chini ya umri wa miaka 25 bado hawana huduma ya mtandao nyumbani,na wasichana wanauwezo mkubwa wa kukosa huduma hiyo.

Aidha alisema pengo la kijinsia kwa watumiaji wa mtandao ulimwenguni lilikua kutoka 11% mwaka 2013 hadi 17% mwaka 2019,katika nchi zilizoendelea zaidi duniani huzunguka karibu 43%.

No comments:

Post a Comment