DC MOYO ACHOMA NYAVU ZA KUVULIA SAMAKI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday 9 September 2021

DC MOYO ACHOMA NYAVU ZA KUVULIA SAMAKI

Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akichoma jumla ya nyavu haramu themanini (80) za kuvulia samaki katika bwawa la Mtera zenye thamani ya shilingi 13,814,000 katika kijiji cha migoli kata ya migoli.

Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akichoma jumla ya nyavu haramu themanini (80) za kuvulia samaki katika bwawa la Mtera zenye thamani ya shilingi 13,814,000 katika kijiji cha migoli kata ya migoli.

Na Fredy Mgunda, Iringa

MKUU wa Wilaya ya Iringa, Mohamed Hassan Moyo amechoma jumla ya nyavu haramu themanini (80) za kuvulia samaki katika bwawa la Mtera zenye thamani ya shilingi 13,814,000 ambazo zimekamatwa katika kipindi cha mwezi wa saba 2021 hadi mwezi wa tisa mwa 2021 ambazo zimekuwa zikitumika katika uvuvi harama katika bwawa hilo.

Akichoma nyavu hizo mkuu wa wilaya huyo alisema kuwa kumekuwa na tabia ya baadhi ya wavuvi kuvua samaki kwa kutumia njia harama ambazo zimekuwa zikileta madhara katika kuazaliana na kukua kwa samaki katika bwawa hilo.

Alisema kuwa sio mara ya kwanza kuchoma nyavu hizo harama kwenye bwawa hilo la Mtera kwani katika kipindi cha mwezi wa saba mwaka 2020 hadi mwezi wa nane mwaka 2021 uongozi wa Halmashauri wa wilaya ya Iringa ulikamata jumla ya nyavu haramu 11,538 zenye thamani ya shilingi 152,100,000.

Moyo alisema kuwa kwa kipindi hicho chote wamekuwa wakikamata nyavu aina ya Timba, Kokoro, Gonga, Kimila na nyavu chini ya nchi tatu  ambazo mara nyingi ndio zimekuwa zikitumiwa na wavuvi haramu katika bwawa hilo la Mtera na kuasababisa uchumi wa wananchi kuyumba kwa kiasi kikubwa.

Alisema kuwa wamekuwa wakitoa elimu ya usimamizi shirikishi wa kulinda rasilimali za uvuvi na kudhibiti uvuvi haramu imekuwa ikitolewa mara kwa mara kwa wavuvi ambapo zaidi ya wavuvi 249 na vikundi 5 vya BMU, wafanyakazi 103 wa samaki wamefanikiwa kupata elimu ya udhibiti wa usafirishaji wa samaki wachanga kwa mujibu wa sheria ya uvuvi ya mwaka 2003 na kanuni zake za mwaka 2009.

Aidha Moyo alisema kuwa katika kuimarisha udhibiti wa wavuvi haramu na ulinzi wa rasimali za uvuvi katika bwawa la Mtera kwa sasa limekuwa shirikishi na jamii kwa kuunda kikosi kazi cha kudhibiti uvuvi Haramu kwa kuwa jamii hiyo inawajua wavuvi haramu na ni kazi rahisi kuwadhibiti chini ya uongozi wa kata, mkuu wa kituo cha polisi migoli na afisa uvuvi wa kata ya Migoli.

Moyo alimalizia kwa kusema kuwa lengo la kuunda kikosi kazi hicho ni kulinda samaki waliopo katika bwawa la mtera ambao ndio wamekuwa wamekuwa tegemeo kwa uchumi wa wananchi wa kata ya Migoli na maeneo ya jirani hivyo bila mikakati maalumu samaki hao watapotea katika bwawa hilo.

Kwa upande wake diwani wa kata ya Migoli Benito Kuyugwa alisema kuwa kutokana na uvuvi haramu kumesababisha kushuka kwa uchumu wa wananchi wa kata hiyo na baadhi ya wananchi wa kuyakimbia makazi yao kutokana na sababu za kiuchumi.

Kuyugwa alisema kuwa migori ya sasa sio ya miaka ya nyuma kutokana na wananchi wake kushuka kiuchumi kutokana na baadhi ya wavuvi kuvua samaki kwa njia haramu ambazo zimesababisha kupungua kwa kuzaliana kwa samaki katika bwawa la Mtera na kushusha uchumi wa wananchi ambao wamekuwa wanategemea uvuvi kuendesha maisha yao.

Kuyugwa alisema kuwa wamefanikiwa kuunda kikosi cha watu 64 ambacho kitapambana na uvuvi haramu na kuwakamata wavuvi na zana zao zote ambazo wanazitumia katika kuvua samaki haramu kwenye bwawa hilo.

Aliiomba serikali kuendelea na doria za mara kwa mara ili kukomesha uvuvi haramu ambao kwa kiasi kikubwa umerudisha nyuma maendeleo ya wanananchi wa kata ya migoli na maeneo mengine yanayolizinguka bwawa hilo.

Kwa upande wake afisa mifugo na uvuvi wa halmashauri ya wilaya ya Iringa methew Sanga alisema kuwa kwa kipindi cha mwezi wa saba 2021 hadi mwezi wa tisa mwa 2021 wamefanikiwa kuwakamata wavuvi kumi na moja (11) na wavuvi tisa (9) wamelipa faini na kuachiwa huku wavuvi wawili (2) wameshindwa kulipa faini hadi hivi sasa wapo maabusu wakisubili huku kwa kuwa tayari walikiri makosa yao kwa kukubari kufanya vitendo hivyo vya uvuvi haramu.

Alisema kuwa serikali imepata boti moja kwa ajili ya doria ya kuwabaini wavuvi haramu ambao wamekuwa walivisumbua vyombo vya ulinzi vya bwawa hilo hivyo uwepo wa boti hiyo kutasaidia kupunguza kwa kiasi kikubwa uvuvi haramu katika bwawa hilo la Mtera.

Sanga alimalizia kwa kusema kuwa serikali ya Halmashuri ya wilaya ya Iringa imetoa elimu kwa viongozi wa serikali,wavuvi na wasafirishaji 121 kwa lengo la kudhibiti uvuvi haramu kwa kuzingatia sheria ya uvuvi namba 22 ya mwaka 2003 na kanunuzi zake za mwaka 2009 ambapo zinamtaka kila mmoja kufanya biashara wakiwa na leseni za uvuvi na biashara ya samaki pamoja na matumizi ya nyavu zenye nchi 3 ili kutovua samaki wachanga.

No comments:

Post a Comment