Meneja wa Bodi ya Mfuko wa Barabara Bw. Eliud Nyauhenga (katikati) akitoa maelekezo kwa watendaji wa TANROADS Mkoa wa Pwani alipokuwa katika ziara hiyo jana. |
Viongozi na wajumbe kutoka Bodi ya Mfuko wa Barabara (RFB) pamoja na watendaji wengine wa TANROADS wakiendelea na ziara yao jana. |
Viongozi na wajumbe kutoka Bodi ya Mfuko wa Barabara (RFB) pamoja na watendaji wengine wa TANROADS wakikagua ujenzi na maendeleo wa Daraja jipya la Wami linaloendelea na ujenzi. |
Bw. Haule ametoa kauli hiyo jana, alipokuwa akikagua ukarabati wa barabara katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Tanga huku akisisitiza hatua za haraka kuchukuliwa kusafisha na kujenga mifereji na madaraja katika maeneo ya Mbezi beach, Tegeta, Boko na Bunju ili mvua zitakapoanza zisisababishe mafuriko na uharibifu wa barabara katika maeneo hayo.
"Shirikianeni na Serikali za mitaa ili watu wanaotiririsha maji machafu, kutupa taka pembezoni mwa barabara na kwenye madaraja wawajibishwe", amesisitiza Mwenyekiti huyo RFB.
Akikagua ukarabati mdogo wa Daraja la Mpiji linalounganisha Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani amemtaka msimamizi wa mradi huo kuhakikisha unakamilika katika kipindi cha mwezi mmoja ujao ili kuondoa usumbufu katika eneo hilo.
Mwakilishi wa Meneja wa TANROADS Mkoa wa Dar es salaam, Bw. Elisius Mtenga amesema takriban kiasi cha shilingi milioni788 zimetengwa kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu ya barabara na madaraja kati ya eneo la mbezi beach hadi Bunju na hivyo maeneo yote yaliozibwa kwa uchafu yatakarabatiwa kabla ya mvua za vuli kuanza.
Meneja huyo amewataka wananchi kujenga tabia ya usafi na kuheshimu maeneo ya barabara na hifadhi zake ili kuzilinda na kuzifanya zidumu kwa muda mrefu.
Katika hatua nyingine RFB imekagua ujenzi wa Daraja jipya la Wami lenye urefu wa mita 510 na barabara za maingilio zenye urefu wa km 3.8 na kuridhishwa na maendeleo ya ujenzi huo. "Ongezeni kasi ya ujenzi watanzania wanasubiri mradi huu kwa fahari kubwa," amesema Bw. Haule.
Naye Meneja wa TANROADS Mkoa wa Pwani, Eng. Andrea Kasamwa ameihakikishia Bodi ya Mfuko wa Barabara kuwa wamejipanga kuhakikisha mradi huo unakuwa bora na kulindwa ili udumu kwa muda mrefu.
Kwa upande wake, Meneja wa Bodi ya Mfuko wa Barabara Bw. Eliud Nyauhenga amesema bodi hiyo iko katika ziara ya kukagua miundombinu ya barabara na madaraja katika mikoa ya Dar es salaam, Pwani na Tanga ili kujiridhisha kama fedha inazotoa kwenye miradi ya barabara zinatumika ipasavyo na kushauri pale inapobidi.
Zaidi ya shilingi bilioni 67.7 zinatarajiwa kutumika katika ujenzi wa daraja jipya la wami.
No comments:
Post a Comment