Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dkt. Jabiri K. Bakari akizungumza NA Washiriki
katika Mkutano wa Madau, Maudhui ya Utangazaji-Jijini Dodoma. |
Washiriki katika Mkutano wa Madau, Maudhui ya Utangazaji. |
SERIKALI imehimiza watoa huduma za Mawasiliano Nchini, kuzingatia Sheria na Kanuni zilizomo kwenye Leseni katika Utoaji wa huduma husika kwa Wananchi.
Akizindua kikao cha Watoa Huduma za Utangazaji na
Maudhui Jijini Dodoma Tarehe 28-07-2021, wadau kutoka Azam Media, Multchoice
Tanzania limited, Watoa Huduma kwa njia ya Cable, COSOTA na TFF ni baadhi ya
washiriki waliohudhuria ambapo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
(TCRA) Dkt. Jabiri K. Bakari, amesema baadhi Kanuni za Maidhui na Utangazaji
zinafanyiwa maboresho na zinatarajia kuanza hivi karibuni
Dkt. Jabiri amesema kuwa TCRA imeboresha utendaji kazi
zake kwa kuweka mifumo madhubuti zaidi na imeendelea kutoa ushauri kwa watoa
huduma kila mara. Kikao hichoshirikishi pia kilihudhuliwa na watoa huduma za
utangazaji na maudhui kutoka vyombo vya habari mbalimbali.
Kikao hicho ambacho kimeratibiwa na Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania (TCRA) kanda ya kati, kililenga kutoa elimu ya namna bora
zaidi katikakufikisha maudhui kwa walaji bila kuwa na migongano baina ya watoa
huduma. Pia kikao kimependekeza wanaochakata maudhui kuangalia namna nzuri zaidi
ya kuzuia maudhui yasiyo na staha kwa Jamii ili kuondoa malalamiko ndani yaJamii.
Kikao kimependekeza pia vikao kama hivi viwe vinafanywa mara kwa mara
ili kuongeza ufahamu zaidi kwa watoa huduma na Mamlaka za
Serikali zinazosimamia sekta ya maudhui ya Utangazaji.
No comments:
Post a Comment