MISAADA, MIKOPO AFRIKA YAGEUZWA KUWA SADAKA YA SHUKRANI KWA MUNGU BABA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday, 9 July 2021

MISAADA, MIKOPO AFRIKA YAGEUZWA KUWA SADAKA YA SHUKRANI KWA MUNGU BABA

 

BABA HALISI katika moja ya Ibada zake kwa ajili ya utukufu wa chanzo halisi.

KUNA maajabu ambayo wataalam wa maendeleo wanayaita Phenomenon! kila  

Bara, Kaskazini ni matajiri na Kusini ni maskini. Kwa mujibu wa Kitabu cha Mwanzo 27:27-40, Baraka huwa ni Moja; Shamba ni Moja; Bustanini Moja; Moyo ni mmoja na zaidi ya yote, CHANZO CHA MEMA NA MAZURI, yaani MUNGU BABA ni Mmoja.

Wote tukifahamu hayo, ugomvi na vita kila mahali itakuwa hakuna.

Katika Mwanzo 25:24-26, Yakobona Esau walizaliwa wakiwa mapacha kutoka katika Tumbo Moja. Yakobo alikuwa wa pili kuzaliwa, ni Mweusi alikuja Kusini. Esau alikuwa wa kwanza kuzaliwa,aliendaKaskazini.

Yakobo, aliyekujaKusini, mahaliambapokatikakila Bara nimaskini, ndiyealiyekuwawa kwanza

Kubarikiwa kwakupewa yaliyo manono ya nchi, mazuri ya umande wa Mbingu, na kwamba kila atakaye mlaani alaaniwe nakila atakaye mbariki a barikiwe. Esau, alipewa Baraka kama hizo alizopewa Yakobo, lakiniyeyealiambiwaatazipatakwaupanga! Yote haya nikwa mujibu waMwa.27:27-40.

Esau, baada ya kuona amepewa Baraka lakini kwa Upanga, alitafuta mbadala wakupata Baraka hizo kutoka kwenye shamba lilelile, bustani ileile, moyo ule ule.

Mbadala huo wakupata baraka Tunausoma katika Matendoya Mitume 20:35.Esau aliposoma katika Matendo ya Mitume 20:35, alikuta imeandikwa kuwa “ni Heri kutoa kuliko kupokea”. Hivyo, Esau akajua Heri ni sawasawa na ile Baraka ambayo hakuipata moja kwa moja.

 Aliamua kujikita katika kutoa misaada na mikopo ndio ukawa upanga wake.

Yakobo, kwakuwa alipewa kilakitu alijikuta nimvivu wakutoa. Katika kitabu cha Warumi 2:9-10, Esau alikuta mahali palipoandikwa kuwa, anayependa kutoa anapata Amani, Heshima na Utukufu. Asiyependa kutoa atapata dhiki na shida.

Esau, aliposoma tena katika Wafilipi 4:16-19, akagundua kuwa Yakobo amekataa kumtunza Mtume Paulo, ndipo Esau akaamua kumtunza Paulo.

Mtume Paulo katikaWafilipi 4:19 akamtamkia Esau kuwa apate kila anachokihitaji kwa kadri yautajiri wa MUNGU wa Majira Saba.

Ndicho kilichotokea kwa Esau. Kwa kuwa Yakobo hakutenda mema, yeye akapata dhiki na s hida katika majira hizo saba.

MUNGU BABA ambaye ni CHANZO HALISI CHA MEMA NA MAZURI amekuja, kwa mujibu wa 1Wakorintho 15:24-28,

Amekuta watoto wawili ambao ni Yakobo na Esau, mmoja anapenda kutoa na amepata Amani, heshima na utukufu, ila kwa mujibu waMwanzo 27:27-40 hakupata Baraka.

Yakobo, yeye alibarikiwa ila hapendi kutoa, matokeo yake akajikuta amepata dhiki na shida! Yakobo ndiye amepata upendeleo wakumpokea MUNGU BABA ambaye ni CHANZO CHA MEMA NA MAZURI, ila hapendi kutoa na ana dhiki na shida.

 Esau ambaye hakubarikiwa kwamujibu waMwanzo 27:27-40, MUNGU BABA hakushukia kwake. Kwa mujibu waWaefeso 4:4-6, huyu MUNGU BABA aliye CHANZO CHA MEMA NA MAZURI anawapenda Yakobo na Esau. Kitu gani afanye?

Jibu sahihi ni kugeuza misaada na mikopo kutoka kwa Esau iwe shukrani kwa MUNGU BABA, ili Yakobo na Esau wote sasa wapate Baraka kutoka kwa Aliye Chanzo cha Baraka.

Yakobo (Kusini) anaye CHANZO CHA MEMA NA MAZURI ila hapendi kutoa. Esau (Kaskazini) hana CHANZO CHA MEMA NA MAZURI ila anapenda kutoa. Ili MUNGU BABA Aliye CHANZO CHA MEMA NA MAZURI, ahudumie wote (Efeso 4:4-6), ili kuwa nilazima amalize ugomvi na vita kati ya hawa wawili kwakugeuza misaada na mikopo kutoka kwa Esau kuwa shukrani kwake. Sasa Yakobo (Kusini) hadaiwi tena maana ule upanga aliopewa Esau haupo.

Wote wawili wanapata kutoka kwa MUNGU BABA–CHANZO HALISI.

Hili halikwepeki maana hata Musa alioa Afrika (Hesabu 12:2-8). Yesu baada yakuzaliwa, alihifadhiwa Afrika ili apone(Mathayo 2:1-15). Yesu pia wakati wakubebeshwa msalaba alisaidiwa na Afrika(Marko 15:21 na Luka 23:26). Lakini pia

Majira sahihi imerejeshwa na aliyetoka Mashariki Halisi (Tanzania –Afrika) katika Isaya 41:2,4. Kwa kuwa huwezi kufanya chochote bila Majira, basi Esau na Yakobo wote wanamhitaji huyu MUNGU BABA aliye CHANZO HALISI CHA MEMA NA MAZURI.

Ndiyo maana ilikuwa nilazima kusawazisha ili Esau na Yakobo wasigombane tena. Hii inamaana kuwa misaada na mikopo ambayo Afrika iliwahi kupata kwa Esau haidaiwi tena. Heri uliyebarikiwak uliko wote.

Mwaandishi wa Makala haya ni Mkuu wa Vituo vyote vya Kanisa Halisi la MUNGU BABA lenye makao makuu yake Tegeta Dar es Salaam Tanzania, BABA HALISI.

No comments:

Post a Comment