Na Dotto Mwaibale, Singida
MBUNGE wa Singida Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Musa Sima amewataka vijana wa chama hicho kuwa wazalendo na kufanya kazi kwa bidii.
Sima ambaye alikuwa mgeni rasmi alitoa ombi hilo wakati akizungumza katika kikao cha kawaida cha Baraza la Vijana wa chama hicho Wilaya ya Singida Mjini kilichofanyika leo.
Sima aliwasisitiza vijana hao kuwa wamoja na kujishughulisha na shughuli za ujasiriamali ili kuinua uchumi wao pamoja na kujiunga na vyuo vya ufundi kama VETA na FDC ambavyo vinatoa mafunzo ya ufundi bure kama alivyoagiza Rais Samia Suluhu Hassan.
Aidha Sima aliwataka vijana hao kuwa makini na matumizi ya mitandao ya kijamii (Social media) ambayo inaweza kuharibu amani ya nchi iwapo itatumiwa vibaya.
Sima alitumia nafasi hiyo kkuwashukuru vijana hao kwa kushiriki vema kwenye uchaguzi mkuu na kuhakikisha chama hicho kinapata ushindi mkubwa
Viongozi wengine waliohudhuria kikao hicho ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya hiyo Lucia Mwiru, Katibu wa CCM wa wilaya hiyo, Shabani Kalage , Katibu wa UVCCM Mkoa Singida George Silindu na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida, Yagi Kiaratu.
No comments:
Post a Comment