Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye kikao kazi alipotembelea Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea (TFRA) akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja Jijini Dar es salaam, Tarehe 7 Juni 2021. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo).
Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda akiakiongoza kikao kazi wakati alipotembelea Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea (TFRA) akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja Jijini Dar es salaam, Tarehe 7 Juni 2021.
Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda akimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Ndg Andrew Massawe akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye kikao kazi alipotembelea Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea (TFRA) akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja Jijini Dar es salaam, Tarehe 7 Juni 2021.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Ndg Andrew Massawe akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye kikao kazi kilichoongozwa na Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda alipotembelea Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea (TFRA) akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja Jijini Dar es salaam, Tarehe 7 Juni 2021.
Sehemu ya Maafisa wa Serikali kutoka Wizara ya Kilimo na TFRA wakifuatilia kikao kazi kilichongozwa na Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda wakati alipotembelea Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea (TFRA) akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja Jijini Dar es salaam, Tarehe 7 Juni 2021.
Na Mathias Canal, Dar es salaam
BODI na Menejimenti ya
Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) imetakiwa kuanisha mkakati wa
upatikanaji wa mbolea nchini kwa bei nafuu.
Waziri wa Kilimo Mhe Prof.
Adolf Mkenda ametoa rai hiyo wakati akizungumza kwenye kikao kazi alipotembelea
taasisi hiyo kujionea hali ya utendaji na upatikanaji wa mbolea wakati akiwa
katika ziara ya kikazi ya siku moja Jijini Dar es salaam.
Pamoja na kuandaa mkakati wa
urahisishaji wa upatikanaji wa mbolea, Pia Waziri Mkenda ameitaka taasisi hiyo
kuandaa mkakati wa uanzishwaji wa viwanda vipya vya mbolea ili kuongeza
uzalishaji wa pembejeo hiyo hapa hapa nchini.
Waziri Mkenda, amesema Bodi
na Menejimenti ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea, ina jukumu kubwa la
kuhakikisha kuwa uzalishaji wa ndani wa mbolea, unapewa kipaumbele na kwa
kuongeza uanzishwaji wa viwanda vipya; mbolea itakuwa ikipatikana kwa urahisi,
nafuu na kila Mkulima atamudu kuinunua na kuitumia.
Prof. Mkenda ameongeza kuwa
Bodi na Menejimenti ya TFRA ibuni mkakati wa namna bora ya kuongeza uwekezaji
hapa hapa nchini, kwa kuwa hilo ndiyo suluhisho la kweli katika kuwahakikishia
Wakulima wengi wadogo unafuu bei.
Kadhalika, amewataka
Watumishi wa TFRA kuongeza udhibiti kwenye usimamizi wa ubora wa mbolea hususan
kwenye mikoa yenye matumizi makubwa ya mbolea.
No comments:
Post a Comment