SERIKALI YASEMA MAANDALIZI YA UMITASHUMTA, UMISSETA YAKAMILIKA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Sunday 6 June 2021

SERIKALI YASEMA MAANDALIZI YA UMITASHUMTA, UMISSETA YAKAMILIKA


Wanafunzi kutoka Mkoa wa Manyara wakiwasili kwenye Shule ya Sekondari ya Ufundi Mtwara leo Juni 6, 2021 tayari kushiriki mashindano ya UMITASHUMTA na UMISSETA yatakayofunguliwa jumanne ijayo na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa kwenye kiwanja cha Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.


Wanafunzi kutoka Mkoa wa Iringa wakipiga ngoma wakifurahia kuwasili leo asuburi Juni 6, 2021 tayari kushiriki mashindano ya UMITASHUMTA na UMISSETA yatakayofunguliwa jumanne ijayo na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa kwenye kiwanja cha Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.



Kamati ya maandalizi ikiweka chokaa kwenye mistari itakayotumika kwa ajili ya riadha kwenye kiwanja cha Sekondari ya Ufundi mjini Mtwara katika mashindano ya UMITASHUMTA na UMISSETA 2021.


Na John Mapepele, Mtwara

KAMATI ya kitaifa ya Mashindano ya Michezo na Taaluma kwa Shule za Msingi (UMITASHUMTA) na Sekondari (UMISSETA) imesema leo kwamba maandalizi kwa ajili ya ufunguzi wa mashindano hayo yatakayofunguliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara. Juni 8,2021 yamekamilika.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mwalimu Ephraim Simbeye ambaye ni Mkurugezi wa Usimamizi wa Elimu Ofisi ya Rais TAMISEMI wakati waliopotembelea leo Juni 6, 2021 kukagua miundombinu na viwanja vitakavyotumika kwenye mashindano hayo mjini Mtwara.

“Mashindano haya yatafanyika katika viwanja vya Nangwanda Sijaona, Chuo cha Walimu Mtwara (TTC kawaida) Chuo cha Walimu Ufundi maarufu kama Mwasandube, na Viwanja vya Shule ya Sekondari ya Ufundi Mtwara.” Amefafanua Simbeye

Simbeye amesema tayari mikoa yote kutoka Tanzania Bara na Visiwani imeshaanza kuleta wanamichezo hao ambapo hadi sasa zaidi ya wanamichezo kutoka mikoa kumi wameshawasili tayari kushiriki mashindano hayo.

“Tunamshukuru Mungu maandalizi yote yanakwenda vizuri na mwitikio wa ushiriki na hamasa ni kubwa, tunategemea mambo makubwa zaidi mwaka huu” amesisitiza Simbeye

Naye Mwenyekiti Mwenza wa mashindano hayo Yusufu Singo ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya michezo nchini kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo amesema mashindano haya yatasaidia kuvumbua vipaji na hivyo kupata wachezaji bora wa timu za Taifa kwa Michezo mbalimbali 

Ameishukuru Serikali kwa kushirikisha Wizara tatu za Habari, TAMISEMI na Elimu kuratibu, kuandaa na kufanya mashindano haya ambapo amesema kwamba huo ni mkakati mzuri utakaosaidia kukuza sekta ya michezo kwa kasi.


Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Ishegoma Emmanuel Ishengoma amesema wasanii  mbalimbali maarufu wa kizazi kipya, taarabu  na singeli wamealikwa  ili  kutoa hamasa na kuwaburudisha wadau mbalimbali kwenye mashindano ya  mwaka huu.

Amewataja baadhi ya wasanii wakaokuwepo kuwa ni pamoja na Zuchu, Peter Msechu, Becka Fleva, Lina sanga Mzee Yusufu na Dula Makabila.

Dkt. Ishengoma ametoa wito kwa wadau mbalimbali nchini kuja kujionea ubunifu na burudani kabambe  itakayotolewa kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania tangia kuanzishwa kwa mashindano haya.


No comments:

Post a Comment