Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge akimuapisha Mkuu Mpya wa Wilaya ya Iramba Selemani Mwenda baada ya kuteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan kushika wadhifa huo.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge akimkabidhi Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ( CCM) Mkuu Mpya wa Wilaya ya Iramba Semani Mwenda baada ya kumuapisha.
Mkuu Mpya wa Wilaya ya Iramba Semani Mwenda akizungumza baada ya kuapishwa.
Familia ya mkuu huyo mpya wa wilaya ya Iramba ikiwa kwenye hafla ya uapisho wa mpendwa wao.
Hafla ikiendelea.
Hafla ikiendelea.
iongozi wa dini wakiwa kwenye hafla hiyo ya uapisho wa mkuu huyo wa wilaya.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge, (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa wilaya ya Singida Mhandisi Paskas Muragili(kushoto) Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Jerry Muro (kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Iramba Selemani Mwenda (wa pili kushoto) baada ya kumuapisha na wa pili kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dorothy Mwaluko.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.Binilith Mahenge akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu Mpya wa Wilaya ya Iramba Selemani Mwenda na familia yake.
Mkuu Mpya wa Wilaya ya Iramba Selemani Mwenda akiwa katika picha ya pamoja na familia yake.
Na Dotto Mwaibale, Singida.
MKUU wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge amesema ishara ya utawala uliotukuka ni amani na utulivu katika maeneo ya kazi na si vinginevyo.
Dkt.Mahenge ameyasema hayo jana baada ya kumuapisha Mkuu Mpya wa Wilaya ya Iramba Selemani Mwenda ambaye ameteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuongoza wilaya hiyo.
"Jambo la msingi ninalopenda kukuambia hakikisha kuna amani na utulivu katika wilaya yako hata ukifanya makubwa mazuri kiasi gani kama hakuna amani na utulivu mambo hayo yatafunikwa na makosa," alisema Mahenge.
Alisema ni wajibu wa viongozi kuhakikisha ulinzi, usalama na amani vinatamalaki muda wote kuzunguka maeneo yao.
Aliongeza kwamba kazi ya kiongozi wa umma, pamoja na mambo mengine ni kuhamasisha maendeleo katika kila nyanja.
"Niwaombe sana vijana wangu wakati mnatekeleza majukumu yenu zingatieni akili za kuambiwa changanya na za kwako," alisema Dkt. Mahenge.
Mahenge aliahidi kuwapaka ushirikiano wakuu wote wa wilaya mkoani hapa lakini kwa wale watakao kuwa wachapa kazi na kuwa afadhari watofautiana kwenye misingi ya utekelezaji wa kazi watakaa na kuamua kipi wakifanye na si majungu.
Akizungumza baada ya kuapishwa Selemani Mwenda alitoa shukurani kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini kushika nafasi hiyo na kuahidi kukidhi matarajio ya nafasi hiyo kwa kwenda kuwatumikia wananchi wa Iramba na kufuata kiapo alichoapa cha utumishi.
Mkuu wa wilaya ya Singida, Mhandisi Paskas Muragili na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Jerry Muro wakizungumza kwa nyakati tofauti katika hafla ya kumpokea Mwenda waliahidi kumpa ushirikiano wakati wa kutekeleza majukumu yake ya kuwaletea wananchi wa Wilaya ya Iramba maendeleo.
No comments:
Post a Comment