WAPENI VIPAUMBELE WANANCHI KATIKA MIRADI YA UJENZI – WAITARA - THE HABARII

THE HABARII

HABARI | MATUKIO | MICHEZO.


ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday, 10 May 2021

WAPENI VIPAUMBELE WANANCHI KATIKA MIRADI YA UJENZI – WAITARA

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhe. Mwita Waitara (wa pili kulia mbele) na Mbunge wa Mtwara Mjini Hassan Mtenga (wa pili kushoto), na Meneja wa Wakala wa Barabara Mkoa wa Mtwara, Eng. Dotto John (katikati) wakikagua maendeleo ya upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Mtwara ambao ujenzi wake unaendelea kwa sasa.



Kazi ya ukarabati wa Barabara ya Nagaga – Masasi ambayo ni sehemu ya Barabara Kuu ya Mtwara – Nanyamba – Tandahimba – Newala – Masasi Km 210 ikiendelea.



Muonekano wa njia ya kuruka na kutua ndege katika Uwanja wa Ndege wa Mtwara ambao ujenzi wake unaendelea kwa sasa.



Meneja wa Wakala wa Barabara Mkoa wa Lindi, Eng. Efatha Mlavi akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhe. Mwita Waitara (wa pili kushoto) alipokagua maendeleo ya ujenzi wa Barabara Ruangwa – Nanganga Km 53 ambayo ujenzi wake kwa kiwango cha lami unaendelea.



Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhe. Mwita Waitara akisisitiza jambo kwa viongozi na watendaji mkoani Mtwara mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Mtwara ambao ujenzi wake unaendelea kwa sasa.



Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhe. Mwita Waitara akitoa maelekezo kwa Meneja wa Wakala wa Barabara Mkoa wa Mtwara, Eng. Dotto John alipokagua maendeleo ya Barabara ya Mtwara - Mnivata Km 50 ambayo ujenzi wake kwa kiwango cha lami umekamilika mkoani Mtwara. 




Muonekano wa Barabara ya Mtwara - Mnivata Km 50 ambayo ujenzi wake kwa kiwango cha lami umekamilika mkoani Mtwara. 




Meneja wa Wakala wa Barabara Mkoa wa Mtwara, Eng. Dotto John akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhe. Mwita Waitara alipokagua maendeleo ya Barabara ya Mtwara - Mnivata Km 50 ambayo ujenzi wake kwa kiwango cha lami umekamilika mkoani Mtwara. 


Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhe. Mwita Waitara akitoa maelekezo kwa Meneja wa Wakala wa Barabara Mkoa wa Mtwara, Eng. Dotto John alipokagua maendeleo ya Barabara ya Mtwara - Mnivata Km 50 ambayo ujenzi wake kwa kiwango cha lami umekamilika mkoani Mtwara. 


NAIBU Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhe. Mwita Waitara amewataka viongozi wa mikoa ya Mtwara na Lindi wanaosimamia kazi za ujenzi wa barabara na viwanja vya ndege kutoa vipaumbele vya ajira kwa wananchi.

Amesema hatua hiyo licha ya kuwawezesha kiuchumi wananchi pia itawafungamanisha wananchi hao na miradi hiyo na hivyo kuwafanya wawe walinzi wazuri wa miradi kwa muda wote na kuiwezesha kudumu kwa muda mrefu.

“Meneja hakikisha unashirikiana na viongozi wenzako ili kuwatambua wananchi wazalendo na wenye uwezo wa kufanya kazi kwa bidii na uaminifu ili wapate ajira…,” amesema Waitara.

Naibu waziri huyo amesema Serikali imepanga kufungua miundombinu ya mikoa ya Lindi na Mtwara kwa kuboresha Bandari, Uwanja wa Ndege wa Mtwara na Barabara ya Mtwara – Nanyamba – Tandahimba – Newala – Masasi yenye urefu wa kilomita 210 ili kuhuisha huduma za kilimo na hatimaye kukuza uchumi wa maeneo hayo.

“Fanyeni kazi kwa bidii, ongezeni kasi ya kilimo cha mazao ya chakula na biashara kwasababu miundombinu hii ikikamilika itavutia wawekezaji wengi kuja kuwekeza na kuchochea ukuaji wa uchumi kwa wananchi kwa ujumla,” amesisitiza Naibu Waziri huyo.

Kwa upande wake Mbunge wa Mtwara Mjini, Mhe. Hassan Mtenga ameitaka Serikali ikamilishe miradi ya ujenzi wa miundombinu katika Ukanda wa Kusini kwa wakati ili kuepuka gharama zisizo za lazima na kuepuka migogoro kati ya Serikali na wananchi hali inayochelewesha baadhi ya miradi.

Naye Meneja wa TANROADS Mkoa wa Mtwara, Eng. Dotto John amemhakikishia Naibu Waziri Waitara kwamba miradi yote ya barabara itakamilika kwa wakati na barabara zitapitika wakati wote, huku Meneja wa TANROADS Mkoa wa Lindi, Eng. Efatha Mlavi akisisitiza kwamba Barabara ya Ruangwa – Nanganga Km 53 inayojengwa kwa kiwango cha lami itakamilika Novemba mwakani.

Naibu Waziri Waitara alikuwa katika ziara ya siku mbili katika mikoa ya Lindi na Mtwara ambapo pamoja na mambo mengine amekagua maendeleo ya miundombinu ya Bandari, Uwanja wa Ndege na barabara.


Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi.


No comments:

Post a Comment