SHINYANGA YAPOKEA MILIONI 167.4 KWA AJILI YA ZOEZI LA KINGATIBA ZA KICHOCHO NA MINYOO YA TUMBO - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday 6 May 2021

SHINYANGA YAPOKEA MILIONI 167.4 KWA AJILI YA ZOEZI LA KINGATIBA ZA KICHOCHO NA MINYOO YA TUMBO

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akifungua kikao kazi Cha uraghibishaji na uhamasishaji wa Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele kwa Viongozi wa Mkoa na Halmashauri zake Kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Shinyanga.

Washiriki wa kila kazi hicho wakiwa Kwenye ukumbi huo ambao ni Wakuu wa Wilaya, wakurugenzi, waganga wakuu wa wilaya, waratibu wa elimu pamoja na waratibu wa NTD wa Halmashauri za Mkoa wa Shinyanga.

Na Catherine Sungura, Shinyanga

MKOA wa Shinyanga umepokea fedha kiasi cha shilingi milioni 167.4 pamoja na kinga tiba kwa ajili ya zoezi la ugawaji wa kinga tiba hizo kwa halmashauri zote  za mkoa huo kwa watoto wenye umri wa kwenda shule.

Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack wakati wa kufungua kikao kazi cha uraghibishaji na uhamasishaji wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kilichoandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Wazee na Watoto kupitia Mpango wa Kudhibiti Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele.

Mhe. Telack amesema mkoa wake umejipanga vizuri  kwa ajili ya kutekeleza zoezi hilo ambalo linatarajia kuanza mwishoni mwa mwezi Mei mwaka huu kwa wanafunzi wote wenye umri wa miaka mitano hadi kumi na nne.

Aidha, Mhe. Telack amewataka Wakurugenzi wa halmashauri zote za  Shinyanga  kuwezesha zoezi la ugawaji wa kinga tiba za Kichocho na Minyoo ya tumbo ili kudhibiti magonjwa hayo na kujenga mazingira mazuri  ya kuhakikisha watoto wote wanafikiwa.

“Magonjwa haya yameathiri jamii yetu na kuleta ulemavu hali ambayo  imeleta usumbuvu kwa wananchi na watoto kutokuweza kuhudhuria vizuri masomo yao vizuri na kupunguza rasiliamali chache tulizonazo”.

Hata hivyo Mkuu wa Mkoa huyo amewahakikishia wananchi kwamba kinga tiba hizo ni salama na zimethibitishwa  na Shrika la Afya Duniani(WHO) na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA) hivyo kuwataka wale wenye imani potofu  kuondoa dhana hiyo.

Vile vile Mhe. Telack amewataka wataalam wa afya na elimu kuwaeleimisha wananchi kwenye maeneo yao kwa kuwapa ujumbe sahihi ili itakapofika zoezi hilo kuweza kutokomeza tatizo hili katika mkoa wao.

Naye Afisa Mradi kutoka Mpango wa Kudhibiti Magonjwa Yaliyokuwa hayapewi Kipaumbele, wizara ya afya Bw. Isaac Njau amesema zipo athari nyingi za muda mfupi na mrefu zitokanazo na kichocho kwa wanaume, wanawake na watoto ikiwemo Udumavu, utapiamlo, kuvimba Ini, kuharibika kwa mimba, Kanda ya kibovu Cha miojo pamoja na upungufu wa Damu mwilini.

 Bw. Njau alitaja Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele  ni pamoja na Usubi,Trackoma,Kichocho,Minyoo ya Tumbo,Matende na Mabusha(Ngirimaji).

No comments:

Post a Comment