RAIS SAMIA SULUHU AHUDHURIA SHEREHE ZA KUAPISHWA RAIS WA UGANDA YOWERI MUSEVENI KAMPALA - THE HABARII

THE HABARII

HABARI | MATUKIO | MICHEZO.


ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday, 12 May 2021

RAIS SAMIA SULUHU AHUDHURIA SHEREHE ZA KUAPISHWA RAIS WA UGANDA YOWERI MUSEVENI KAMPALA

 

Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Museveni akikagua Gwaride la Jeshi la Uganda huku akiwa kwenye Gari la wazi mara baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Uganda katika kipindi cha muhula mwingine katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa Kololo, Kampala nchini Uganda.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na Marais wengine wa Nchi za Kiafrika pamoja na Wageni wengine waliohudhuria sherehe za Uapisho wa Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni zilizofanyika katika Uwanja wa Kololo, Kampala nchini Uganda.




Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Museveni akikagua Gwaride la Jeshi la Uganda huku akiwa kwenye Gari la wazi mara baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Uganda katika kipindi cha muhula mwingine katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa Kololo, Kampala nchini Uganda.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwasili katika Uwanja wa Kololo, kwa ajili ya kuhudhuria Sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni zilizofanyika katika uwanja huo uliopo Kampala nchini Uganda leo tarehe 12 Mei, 2021.



Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Museveni akizungumza mara baada ya kuapishwa katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa Kololo, Kampala nchini Uganda. PICHA NA IKULU.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa katika uwanja wa Kololo Kampala nchini Uganda katika sherehe za Uapisho wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni.



No comments:

Post a Comment