RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS WA KENYA UHURU KENYATTA MARA BAADA YA KUWASILI NAIROBI NCHINI KENYA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday 4 May 2021

RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS WA KENYA UHURU KENYATTA MARA BAADA YA KUWASILI NAIROBI NCHINI KENYA

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta nchini Kenya kwa ajili ya ziara ya siku mbili.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akisaini Kitabu cha Wageni Mara baada ya Kuwasili katika Ikulu ya Nairobi nchini Kenya.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride la Heshima aliloandaliwa na Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF) mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Nairobi nchini Kenya leo tarehe 04 Aprili, 2021.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama pamoja na Rais wa Kenya Uhuru Muigai Kenyatta wakati wa nyimbo za Mataifa Mawili ya Tanzania na Kenya zikipigwa mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Nairobi nchini Kenya leo tarehe 04 Aprili, 2021.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa katika Mazungumzo na Rais wa Kenya Uhuru Muigai Kenyatta mara baada ya kuwasili Nairobi nchini Kenya leo 04 Aprili, 2021.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Rais wa Kenya Uhuru Muigai Kenyatta wakati wakielekea kwenye mazungumzo ya Pamoja na Ujumbe wa nchi mbili Tanzania na Kenya.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta nchini Kenya kwa ajili ya ziara ya siku mbili.

No comments:

Post a Comment