MAWAZIRI, PROF. MKUMBO NA MWAMBE WAKUTANA NA WAZIRI WA UINGEREZA KUJADILI MASUALA YA BIASHARA NA UWEKEZAJI - THE HABARII

THE HABARII

HABARI | MATUKIO | MICHEZO.

ASAS GROUP

Habari Mpya

Tuesday, 11 May 2021

MAWAZIRI, PROF. MKUMBO NA MWAMBE WAKUTANA NA WAZIRI WA UINGEREZA KUJADILI MASUALA YA BIASHARA NA UWEKEZAJI

Waziri wa Viwanda na Biashara, Prof. Kitila Mkumbo na Waziri wa Uwekezaji, Mhe. Geofrrey Mwambe kwa pamoja wakifanya mazungumzo na Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje, Jumuiya ya Madola na Maendeleo ya Uingereza, Bw. James Duddridge.

WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Prof. Kitila Mkumbo na Waziri wa Uwekezaji, Mhe. Geofrrey Mwambe kwa pamoja wamekutana Mei 11, 2021 na kufanya mazungumzo na Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje, Jumuiya ya Madola na Maendeleo ya Uingereza, Bw. James Duddridge.

Katika kikao hicho Mawaziri hao wamepata fursa ya kujadili masuala mbalimbali ya kudumisha na kukuza mahusiano ya biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Uingereza hususani kwa bidhaa muhimu za Tanzania kuuzwa nchini Uingereza na kuvutia Uwekezaji mkubwa wa Uingereza hapa nchini.

Kikao hicho kimehudhuriwa pia na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Prof. Godius Kahyarara pamoja na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Mhe. David Concar.

No comments:

Post a Comment