DKT. ABBASI ATAKA WANAMICHEZO KUJIAMINI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday 3 May 2021

DKT. ABBASI ATAKA WANAMICHEZO KUJIAMINI

 

Hafla ya futari maalum iliyoandaliwa na Kampuni ya Peak Time Media Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mabondia, wadau wa ndondi.



Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi akizungumza kwenye kwenye futari maalum iliyoandaliwa na Kampuni ya Peak Time Media Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mabondia, wadau wa ndondi na pia kumuenzi Rais wa Shirikisho la Ngumi za Kulipwa nchini Tanzania Yassin Abdallah Ustadh.

Na Mwandishi Wetu

 

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi amewataka wanamichezo wote nchini kujiamini wanapokuwa kwenye michezo yao ili waweze kushinda na kulitangaza Taifa letu duniani.

 

Amesema wanamichezo wanapaswa kutambua kuwa wao ni wawakilishi muhimu wa Taifa na kwamba Serikali kwa sasa ipo karibu na wanamichezo na tayari imeshaanza kutenga fedha kusaidia wanamichezo wanaoshiriki michezo mbalimbali ya kimataifa. 

 

Akizungumza jana Mei 2, 2021 kwenye futari maalum iliyoandaliwa na Kampuni ya PeakTime Media Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mabondia, wadau wa ndondi na pia kumuenzi Rais wa Shirikisho la Ngumi za Kulipwa nchini Tanzania Yassin Abdallah Ustadh ambaye alifariki tarehe 7/9/2020 Dkt. Abbasi amesisitiza wanamichezo kujituma na kuwa na nidhamu wakati wote ili kufika mbali.

 

“Serikali kwa sasa haitoi tu bendera kwa wanamichezo, tunatoa pia fedha na vitu vingine kwa ajili ya wanamichezo wetu ili waweze kutuwakilisha vyema kwenye michezo ya kimataifa.” Amefafanua Dkt. Abbasi.

 

Ameongeza kuwa, kwa sasa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imefanya mageuzi makubwa ambapo imeshaondoka kuwa msimamizi tu wa Sera za Sekta za Michezo na kuwa pia  mapromota kabisa wa michezo kama hii ya ngumi Tanzania.

Kwa upande wake muandaaji wa hafla hiyo, Afande suleiman Semunyu ameishukuru Serikali kwa kusimamia na kuwa karibu na wadau karibu na wadau wa michezo na kuahidi kuendelea kushirikiana na Serikali  ili kufanya vizuri zaidi kwenye michezo hiyo.

No comments:

Post a Comment