MASHUA YA KWANZA DUNIANI KUTENGENEZWA KWA TAKA ZA PLASTIKI FLIPFLOPI ILIVYOTUA DAR - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday, 19 April 2021

MASHUA YA KWANZA DUNIANI KUTENGENEZWA KWA TAKA ZA PLASTIKI FLIPFLOPI ILIVYOTUA DAR


MASHUA YA KWANZA DUNIANI KUTENGENEZWA KWA TAKA ZA PLASTIKI FLIPFLOPI ILIVYOTUA DAR

MNAMO mwaka 2016, Ali A. Skanda kutoka Lamu nchini Kenya, pamoja na wenzake wawili kwa waliungana na kutengeneza mashua waliyoiita Flipflopi kwa kutumia taka taka za plastiki zilizokuwa  takribani tani kumi (10) na kuifunika kwa ndala elfu thelasini (30,000), ambapo  mpaka kukamilika kwake  2018, mashua hiyo ilikuwa na uzito wa tani 8, na ndicho chombo cha kwanza cha majini  duniani kutengenezwa kwa takataka za plastiki.

Tarehe 15.04.2021 mashua hiyo ilitua Dar es Salaam ikiwa imebeba ujumbe wa kuhimiza usafi wa mazingira  ya Fukwe za Bahari, Maziwa pamoja   na mito kwa kwa ajili ya usalama wa viumbe wanaoishi humo na afya kwa wanadamu.

 Jumamosi tarehe 17.04.2021 ujumbe huo wa Flipflopi pamoja na wenyeji wao  wa Nipe Fagio waliungana kufanya usafi katika ufukwe wa Minazi Mikinda Kigamboni, na kuweza kukusanya  zaidi ya mifuko 90  ya takataka.

 

Mashua na Boti  ya FlipFlopi  zikiwa katika Bahari ya Hindi eneo la Kigamboni Dar es Salaam

Taasisi  isiyo ya Kiserikali  ya Nipe Fagio kutoka Tanzania kwa kushirikiana na projecti ya Flipflopi pamoja na wakazi mbalimbali wa Dar es Salaam wakiwa katika usafi wa kusafisha ufukwe   wa Bahari  eneo la   Minazi Mikinde Kigamboni wakati ujumbe wa projecti ya FlipFlopi ulipotua Dar es Salaam, Tanzania kwa ajili ya kuhamasisha usafi wa Mazingira ya Bahari hasa kupambana na  taka za plastiki pamoja na taka taka zengine ambazo ni hatari kwa viumbe hai wa Baharini.

Muonekano wa Dampo ambalo sio rasmi, linalosabisha uchafuzi mkubwa wa ufukwe wa  Bahari eneo la Minazi Mikinde Kigamboni ambapo walioshiriki wa kufanya usafi walifanikiwa kupunguza taka hizo kwa kiasi kikubwa.

Zoezi la uchambuzi wa taka likiendelea baada ya kuokotwa kutoka  ufukweni mwa Bahari, zoezi hilo hufanyika ili kuweza kufahamu idadi ya taka zilizopatikana na kufahamu makampuni ambayo yanazalisha bizaa hizo zinazopelekea uchafuzi wa mazingira ya Bahari, katika zoezi la usafi Zaidi ya viroba  80 vya taka vilikusanywa, taka zilizokusanywa ni Pamoja na plastiki, nepi  za Watoto, vifaa vya umeme, nguo, viatu, ndala,  nyavu za Samaki, vifungashio vya vyakula na aina zengine mbalimbali.

 Muonekano wa Ufukwe wa Bahari eneo la Minazi Mikinde Kigamboni kabla na Baada ya   baada ya kufanyiwa usafi.

Maonesho ya bidhaa mbalimbali zinazotokana na urejelezaji wa Taka  rejeshi. Picha na Fredy Njeje.

 

 

No comments:

Post a Comment