SERIKALI YA MAREKANI YAKABIDHI VIFAA TIBA ILI KUPAMBANA NA JANGA LA UVIKO-19 ZANZIBAR - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday 19 April 2021

SERIKALI YA MAREKANI YAKABIDHI VIFAA TIBA ILI KUPAMBANA NA JANGA LA UVIKO-19 ZANZIBAR

Kwa mwaka jana, Marekani imetoa Dola milioni $ 16.4 kupunguza UVIKO-19 nchini Tanzania.

SERIKALI ya Marekani, kupitia Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) ilikabidhi vifaa vya UVIKO-19 kwa Wizara ya Afya ya Zanzibar. Mradi wa USAID wa Mnyororo wa Ugavi wa Afya Duniani hivi karibuni ulinunua vifaa vya upumuaji  na usafi wa mazingira vyenye thamani ya Dola za Marekani  $400,000. 

Vifaa viliwasilishwa mwezi uliopita Bandari ya Zanzibar na kusambazwa kwenye vituo vya umma vya kutolea huduma za afya kupitia bohari kuu ya madawa. Shehena hiyo inajumuisha vifaa vya kupumulia kama vile vipimo vya mwenendo wa damu, mirija ya kupimia puani kwa watoto na watu wazima, barakoa; na vifaa vya usafi wa mazingira kama vile dawa za mkoba za kunyunyizia, na mifuko ya kuwekea taka hatarishi.

Akizungumzia kuhusu utoaji wa vifaa tiba, Dk Abdullah S. Ali, Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto, Zanzibar alisema "Tunaamini katika uhusiano wa ushirikiano ambao unatoa huduma bora za afya kwa watu wote. Shehena ya vifaa tiba vilivyopokelewa vitaziba mapengo yaliyopo katika kupunguza hofu inayohusishwa na tishio la UVIKO- 19 kwa suala la vifo, maradhi na kulazwa hospitalini. ”

Katika miezi ya hivi karibuni, anuwai mpya ya virusi vya korona imesababisha wimbi lingine kali zaidi la maambukizi ulimwenguni, pamoja na bara la Afrika. Imekuwa wazi kuwa virusi viko Tanzania pia. Serikali ya Marekani imejitolea kufanya kazi bega kwa bega na washirika wote katika sekta ya afya ya Tanzania ili kupunguza athari za UVIKO-19. Kwa kipindi cha mwaka mmoja sasa, Marekani imetoa Dola za Marekani milioni 16.4 kupunguza UVIKO-19 nchini Tanzania.


Serikali ya Marekani inafurahi kushirikiana na Wizara ya Afya ya Zanzibar kutoa vifaa hivi muhimu.  Tunakaribisha pia agizo la Rais Samia Suluhu Hassan kwamba ana nia ya kuunda kikosi kazi cha UVIKO-19 na kutoa ushauri wa kisayansi wa namna ya kukabiliana nayo kwa usahihi. Kwa kuongezea, Serikali ya Marekani inatumaini mapitio ya ushahidi wa chanjo ni sehemu ya mchakato huo.

Akizungumza katika hafla ya leo, Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dkt.Donald J. Wright alisema "Chanjo zimesaidia kutokomeza baadhi ya magonjwa mabaya zaidi duniani, na hakuna shaka kuwa kampeni ya chanjo kwa wote ya UVIKO-19 itaokoa maisha."

Balozi Wright aliendelea, "Mbali na kutekeleza tahadhari za msingi za kuzuia kuenea kwa UVIKO-19, ni muhimu kukusanya na kuripoti habari kuhusu upimaji na visa. Kufanya hivyo kunafanya serikali kujua ikiwa hatua za kukabiliana zina matokeo yanayokusudiwa. Kwa kushirkisha taarifa hii kunawahakikishia raia kwamba serikali zao zinapambana kulinda afya zao na maisha yao. ”


Kuomba taarifa zaidi, tafadhali piga simu Ubalozi wa Marekani Ofisi ya Habari Dar es Salaam Simu: +255 22 229-4000 au barua pepe: DPO@state.gov.

No comments:

Post a Comment