VIJANA SINGIDA WAMPONGEZA RAIS MAMA SAMIA SULUHU - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday, 22 March 2021

VIJANA SINGIDA WAMPONGEZA RAIS MAMA SAMIA SULUHU

Kaimu Afisa Vijana Mkoa wa  Singida, Frederick Ndahani.


Na Dotto Mwaibale, Singida

VIJANA  wa Mkoa wa  wamempongeza Mama Samia suluhu  Hassan kwa kula kiapo cha kuwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.

Akizungumza kwa niaba  ya Vijana wa Mkoa wa Singida Kaimu Afisa Vijana wa   mkoa huo, Frederick Ndahani  alisema wana imani kubwa na Rais Samia  kwani kabla ya kushika nafasi hiyo ya juu alikuwa Makamu wa Rais ni Mama anayejua kazi na kujiamini lakini pia anaifahamu miradi yote ambayo ilianzishwa na Hayati John Pombe Joseph Magufuli mfano ujenzi wa Reli ya kisasa, Bwawa la Umeme ,madaraja na uboreshaji wa miondombinu ya barabara katika miji sambamba na uboreshaji wa usafiri wa anga na majini, ujenzi wa  shule,vituo  vya   afya  na hospitali.

" Rais Mama  Samia amekuwa kiungo kikubwa katika kutatua kero za Muungano kwani ameshawahi kuwa Waziri wa Muungano na hata wizara ya Muungano ilikuwa chini yake wakati akiwa Makamu wa Rais, hivyo tunaamini muungano wetu  utazidi kuimarika" alisema Ndahani.

Rais Mama   Samia wakati wa kampeni alitembea nchi nzima kuomba kura katika uchaguzi wa mwaka 2015 na uchaguzi wa mwaka 2020, hivyo anaifahamu vizuri nchi yetu na mahitaji ya watanzania.

Alisema wao kama  vijana wanaahidi kushirikiana vyema katika kipindi chote cha uongozi wake ukizingatia kuwa Rais aliyepita tayari alikwisha wajenga katika misingi ya uzalendo,kufanya kazi pamoja na kuipenda nchi yetu.

Ndahani alisema  wanamuombea Rais Mama Samia Suuluhu Hassani  kwa Mungu ampe  afya njema na baraka katika kipindi chore  cha uongozi wake.

No comments:

Post a Comment