RUWASA NYASA YATATUA KERO YA MAJI KIJIJI CHA CHIMATE - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday, 30 March 2021

RUWASA NYASA YATATUA KERO YA MAJI KIJIJI CHA CHIMATE

Mkuu wa Wilaya ya Nyasa, Mh. Isabela Chilumba, hivi karibuni, aKIweka jiwe la Msingi la Mradi wa Maji Kijiji cha Chimate,  utakaohudumia Wananchi zaidi ya 2798 Wilayani Nyasa ambao umejengwa na Serikali na utagharimu tsh 390,87,000 hadi kukamilika kwake .Mradi huu umetatua tatizo la maji katika kijiji hicho kwa kuwa awali hapakuwa na mradi wa maji.

MKUU wa Wilaya ya Nyasa Mh. Isabela Chilumba, hivi karibuni, ameweka jiwe la Msingi la Mradi wa Maji Kijiji cha Chimate,  utakaohudumia Wananchi zaidi ya 2798 Wilayani Nyasa.


Mradi huu umefikia asilimia 85 ya ukamilishaji wake, na Vituo kumi vya maji vimeshaanza kutoa maji na wananchi wananufaika na huduma ya maji safi na salama, na mpaka kukamilika kwake, Mradi unatarajia kugharimu milioni 390,870,000 Fedha ambazo zimetolewa na Serikali kupitia Mradi wa EP4R.

Akiweka Jiwe la Msingi Mh.Chilumba amewapongeza Ruwasa Mkoa wa Ruvuma na Wilaya ya Nyasa kwa Mradi Mzuri ambao baada ya kukagua ameridhishwa na Ufanisi wa mradi huo kwa kuwa, Mpaka anaweka jiwe la Msingi Mradi unatoa huduma kwa Wananchi, na kuwataka waendeleze juhudi hizo na kuhakikisha wanamaliza Kero ya ukosefu wa maji Wilayani hapa.

Aidha ametoa wito kwa wananchi wa Kijiji cha Chimate kutunza Miundombinu ya Maji ili iweze kuwanufaisha kwa miaka mingi na kutoharibu vyanzo vya maji.

Kwa upande wao, Wananchi wa Kijiji cha chimate Wameipongeza Serikali kwa Kuwajengea Mradi huo ambao umetatua kero ya Maji katika Kijiji hicho kwa Kuwa awali hapakuwa na Huduma ya Maji safi, hali ambayo iliwalazimu kutembea umbali wa takribani kilometa 5 hadi 10 kufuata maji,katika Vyanzo vya asili.

Awali Akitoa Taarifa fupi ya Mradi wa maji kwa Mkuu wa Wilaya ya Nyasa, Mhandisi Jeremia Maduhu amesema Ruwasa Nyasa Imetekeleza mradi huo kwa njia ya Force account na kufanikiwa, kutekeleza mradi huo kwa kuwa mpaka sasa umefikia asilimia 85 na unatarajia kukamilika April 15 mwaka huu.

Amezitaja kazi zilizofanyika ni pamoja na ujenzi wa Temki jipya,  lenye ujazo wa lita 75,000, Ujenzi wa Vituo vya kuchotea maji 18, na Tayari vituo 10 vimeshaanza kutoa huduma ya maji safi kwa wananchi na ujenzi wa mtandao wa bomba za kusambazia maji kilometa 18.53,  kazi ambayo imefanyika na iliyobaki ni kuunganisha ili vituo nane vilivyobabi viweze kutoa huduma ya maji kwa Wananchi wa Kijiji cha Chimate Wilayani Nyasa.


No comments:

Post a Comment