KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MIUNDOMBINU YATEMBELEA MRADI WA MAGOMENI KOTA NA DART - THE HABARII

THE HABARII

HABARI | MATUKIO | MICHEZO.


ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday, 17 March 2021

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MIUNDOMBINU YATEMBELEA MRADI WA MAGOMENI KOTA NA DART

 

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi, Godfrey Kasekenya (wa pili kushoto mbele) pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi) Arch. Elius Mwakalinga (wa kwanza kushoto) akiwaongoza Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu ilipotembelea Mradi wa Ujenzi wa nyumba za makazi kwa waliokuwa wakazi wa Magomeni Kota jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Selemani Kakoso.



Eng. Ladislaus Bigambo kutoka Wizara ya Ujenzi (kulia) akimwelezea Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Selemani Kakoso (katikati) namna mtambo mpya maalum wa ukaguzi wa ubora wa barabara na madaraja unavofanya kazi, wengine ni wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu wakishuhudia.



Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi, Godfrey Kasekenya (wa pili kushoto mbele) akitoa taarifa fupi kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu ilipotembelea Mradi wa Ujenzi wa nyumba za makazi kwa waliokuwa wakazi wa Magomeni Kota jijini Dar es Salaam. 



Meneja wa mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi , Magomeni Kota Benard Mayemba (kulia mbele)
 akiwaeleza wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu namna kiwanda cha kufyatua matofali kinavyofanya kazi walipotembelea Mradi wa Ujenzi wa nyumba za makazi kwa waliokuwa wakazi wa Magomeni Kota jijini Dar es Salaam. 




Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu wakiliangalia gari lililofungwa mtambo mpya wa kisasa unaofanya kazi ya ukaguzi wa ubora wa barabara na madaraja nchini walipotembelea Mradi wa Ujenzi wa nyumba za makazi kwa waliokuwa wakazi wa Magomeni Kota jijini Dar es Salaam. 



Gari lililofungwa mtambo maalum mpya wa kisasa unaofanya kazi ya ukaguzi wa ubora wa barabara na madaraja nchini. 



Meneja wa mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi, Magomeni Kota, Benard Mayemba (kulia aliyesimama) akitoa taarifa fupi ya Ujenzi wa nyumba za makazi kwa waliokuwa wakazi wa Magomeni Kota jijini Dar es Salaam kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu walipotembelea Mradi huo.



Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi) Arch. Elius Mwakalinga (wa pili kushoto) akifafanua jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu ilipotembelea Mradi wa Ujenzi wa nyumba za makazi kwa waliokuwa wakazi wa Magomeni Kota jijini Dar es Salaam. 


Mwonekano wa sehemu ya majengo ya Mradi wa Ujenzi wa nyumba za makazi kwa waliokuwa wakazi wa Magomeni Kota jijini Dar es Salaam. 



Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi) Arch. Elius Mwakalinga akifafanua jambo kwa wanahabari mara baada ya ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu ilipotembelea Mradi wa Ujenzi wa nyumba za makazi kwa waliokuwa wakazi wa Magomeni Kota jijini Dar es Salaam. 



Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi, Godfrey Kasekenya akizungumza na wanahabari mara baada ya ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu ilipotembelea Mradi wa Ujenzi wa nyumba za makazi kwa waliokuwa wakazi wa Magomeni Kota jijini Dar es Salaam. 



Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Selemani Kakoso akizungumza na wanahabari mara baada ya ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu ilipotembelea Mradi wa Magomeni Kota jijini Dar es Salaam. 



Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Patrick Mfugale (kushoto) akitoa taarifa fupi kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu ilipotembelea mradi wa usafiri wa mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam (DART). 

No comments:

Post a Comment