Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Miundombinu Suleiman Kakoso akihoji jambo kwa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile wakati kamati hiyo ilipotembelea katika shirika la Mawasiliano TTCL katikati ni Mkurugenzi wa Shirika hilo Waziri Kindamba.
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile katikati akiongozana na Mwenyekiti wa Kamati ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Mh. Suleiman Kakoso wa pili kutoka kulia wakati kamati hiyo ilipotembelea Mkongo wa mawasiliano wa Taifa unaomilikiwa na shirika la Mawasiliano TTCL kushoto ni Waziri Kindamba Mkurugenzi wa Shirika hilo. |
Mkurugenzi wa Shirika la Mawasiliano TTCL Waziri Kindamba akifafanua jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu wakati wajumbe hao walipotembelea kituo cha Mawasiliano cha Mokongo wa Mawasiliano.
Baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo wakijadiliana jambo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL Bw. Waziri Kindamba akiwaongoza baadhi ya wajumbe wa Kamati ya kudumu ya bunge ya Miundombinu wakati walipotembelea shirika hilo leo.
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile katikati akiongozana na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Miundombinu Suleiman Kakoso wa pili kutoka kushoto kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dk. Jommy Yonaz na Mkurugenzi mkuu wa TTCL Waziri Kindamba.
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile wa pili kutoka kulia akimsikiliza Mwenyelti wa kamati ya Kudumu ya bunge ya Miundombinu Mh. Suleiman Kakoso wakati akizungumza na wanahabari baada ya ziara hiyo kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Waziri Kindamba na kushoto ni Mjumbe wa Kamati hiyo Mbunge wa jimbo la Ikungi Mashariki Mh. Miraji Mtaturu.
Na Adeline Berchimance, Dar es Salaam
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imempongeza Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile kwa kuhakikisha Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano unamilikiwa na Serikali kwa asilimia 100 tofauti na ilivyokuwa awali.
Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mhe. Seleman Kakoso (Mb) wakati wa ziara ya Kamati hiyo kutembelea Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL, Corporation) kwa lengo la kukagua miradi ya maendelea inayotekelezwa na shirika hilo.
Mhe. Kakoso amesema kitendo cha Serikali kumiliki Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kutasaidia kuleta ufanisi kutokana na ukweli kwamba Mkongo ni uchumi na ni muhimu kwa usalama wa Nchi. Ameongeza kuwa kwa jitihada za Waziri mwenye dhamana na Wizara hiyo Serikali imefanya maamuzi ambapo TTCL atalipwa stahiki zake zitokanazo na kuhudumia Mkongo huo tofauti na miaka ya nyuma, ambapo TTCL ilikuwa hailipwi licha ya kutumia gharama kubwa kuhudumia Mkongo huo.
"Ndani ya kipindi cha miezi mitatu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ameweza kufanyia kazi maagizo na maelekezo yaliyotolewa na Serikali. Kamati imeridhishwa na kasi ya ufanyaji kazi wa Serikali kupitia Waziri Ndugulile," alisema Mhe. Kakoso Mwenyekiti wa Kamati.
Aidha, Mhe. Kakoso amesema ndani ya siku mia moja za Wizara mpya ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imetekeleza maagizo ya Serikali ya kuhakikisha Wafanyakazi wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki wanalipwa stahiki zao zote.
Amesema kabla ya maelekezo hayo Shirika la Posta lilikuwa linalazimika kulipa kiasi cha shilingi milioni sabini kwa mwezi kwa Wafanyakazi hao ambapo sasa malipo hayo yakuwa yanafanywa na Hazina na hivyo kuondoa mzigo mkubwa kwa Shirika la Posta.
"Waziri Ndugulile amefanya kazi kubwa Sana, amehakikisha Wafanyakazi wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki wanalipwa na Hazina," amesisitiza Kakoso akizungumza katika ziara hiyo.
Pamoja na pongezi hizo amemtaka Waziri Ndugulile kuhakikisha anasimamia Taasisi na Mashirika yote yanayodaiwa na TTCL pamoja na Shirika la Posta kulipa madeni yote yaliyotokana na kutumia huduma kutoka kwa Mashirika hayo.
Kwa upande wake Waziri Dkt. Faustine Ndugulile amesema maelekezo yaliyotolewa na Kamati hiyo ameyapokea kwa niaba ya Serikali na yataanza kufanyiwa utekeleza mara moja. Amesema wakati wa kuundwa kwa Kamati hiyo yapo maelekezo yaliyotolewa na yalihitaji utekelezaji wa haraka na mengi yametekelezwa ndani ya siku mia moja na mengine yapo kwenye hatua za utekelezaji.
Akizungumza suala la madeni amesema kwa upande wa Posta ilikuwa inaidai Hazina zaidi ya bilioni kumi na Posta ilikuwa inatumia milioni sabini mpaka sabini na tano kuwalipa wastaafu kwa mwezi na sasa taratibu ziko hatua za mwisho na Wastaafu hao watakuwa wanalipwa na Hazina.
Katika kuazimisha siku mia moja za Wizara mpya Mhe. Ndugulile amesema yapo mengi yatafanyika katika siku kumi na tano za maadhimisho hayo ikiwa ni pamoja na kuzindua jengo jipya la Makao Makuu ya Shirika la Posta Afrika, atafanya uzinduzi wa miradi ya minara ambapo katika kipindi hicho Serikali imewezesha Watanzania zaidi ya laki saba kupata mawasiliano ya simu.
Ameongeza kuwa ndani ya siku miamoja zimepatikana fedha zaidi ya Billion moja kwa ajili ya anwani ya makazi na post code na kutatua tatizo la vifurushi ambalo lilikuwa ni tatizo kubwa kwa watumiaji wa Mawasiliano ya simu.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL, Bw. Waziri Kindamba akizungumza na wanahabari mara baada ya ziara hiyo, amebainisha kuwa moja kati ya mafanikio makubwa yaliyopatikana katika kipindi cha siku miamoja za Wizara mpya ni kulipwa kwa kiasi cha shilingi bilioni kumi na moja huku Shirika limeingia makubaliano na wadaiwa kulipa madeni yao kwa awamu mpaka kuisha kwa deni husika.
No comments:
Post a Comment