Mkamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Raphael Chibunda (wa pili kutoka kushoto) Akizungumza na Washindi wa mashindano hayo na wanafunzi wengine walioshiriki kwenye hafla hiyo, Kushoto ni Meneja wa CRDB tawi la SUA Isabela Kitila.
Mkamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Raphael Chibunda (Katikati) akimkabidhi Mshindi wa laptop Megan Manase Mushi laptop yake na kushoto ni Meneja wa CRDB tawi la SUA.
Washindi wa shindano hilo wakiwa kwenye picha ya Pamoja na mgeni rasmi katika hafla hiyo ambaye ni Mkamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Raphael Chibunda pamoja na Viongozi wa CRDB na Viongozi wa Serikali ya Wanafunzi SUA yaani SUASO.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Upande wa Taaluma Prof. Maulid Mwatawala (mwenye tai nyekundu) akiwa Mshauri wa wanafunzi SUA Bwana Pure Mulshabi na viongozi wengine wa SUA na CRDB wakati wa afya hiyo.
Na Calvin Gwabara – Morogoro
MAKAMU wa Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo (SUA) Prof. Raphael
Chibunda amewataka Wanafunzi wa Chuo hicho kufungua akauti katika Taasisi za Kifedha ili kuweza kuwajengea nidhamu ya fedha wanazo
zipata kutoka bodi ya mikopo na kwa Wazazi.
Ushauri huo ameutoa wakati wa hafla fupi ya kukabidhi zawadi kwa wanafunzi
watatu ambao wameshinda zawadi za Tanakilishi mpakato yaani (LAPTOP mbili na Simu
janja moja zilizotolewa na Benki ya CRDB tawi la SUA kutokana na kufanya
miamala mingi kupitia akauti zao za SCHOLAR ACCOUT.
“Mimi niwapongeza kwa kuweza kushinda, nyinyi ni vijana lakini mkae
mkijua ujana unapita na majukumu
yanazidi kuongezeka ni vizuri kujiwekea utamaduni wa kutumia taasisi za kifedha
wale ambao mmeamua kwenda CRDB kungua hizi akauti nawapongeza sana matumiani
yangu ni kwamba hitawajengea nidhamu ya matumizi mazuri ya fedha mnazo zipata”Alisema
Prof .Chibunda.
Prof. Chibunda fedha amesema ambazo wanazipata kutoka kwenye bodi ya Mikopo
ya Elimu ya Juu, amewakumbusha kuwa ni kweli zile ni za mkopo na mkopo siku zote
unapaswa utumike kwa tahadhali na kwa malengo ambayo yamekusudiwa hivyo wawe
makini kwenye matumizi na kukumbuka kuzirudisha wamalizapo chuo ili zisaidia
Watanzania wengine.
Ametumia pia nafasi hiyo kuwakumbusha Wanafunzi wote kuchukua tahadhari
katika wakati huu ambao jamii serikali na wataalamu wa afya wanakumbusha
kuchukua tahadhari zote za maambukizi ya Ugonjwa wa COVID 19 kama ambavyo
inashauriwa na wasifanye mzaha maana Chuoni kuna wanafunzi wengi.
“Sisi kama Chuo tumeweka maji ya kunawa kila kona ya Chuo chetu ili
Wanafunzi waweze kupata huduma za kunawa mikono na tunaomba msipuuze naweni
mikono na msione aibu kuvaa barakoa vaeni kama mnazo ili mjikinge nyinyi na na
kuwakinga wenzenu pia|” Alisisitiza Prof. Chibunda.
Kwaupande wake Meneja wa Benki ya CRDB
tawila la SUA Isabela Kitila amesema CRDB imweza kubuni na kuja na
akauti hiyo ya SCHOLAR ACCOUT ili kuweza kumsaidia Mwanafunzi kipindi anapokuwa
Chuoni katika kipindi chake cha masomo.
“Hii akauti haina makato ya mwezi kwahiyo mwanafunzi anapofanya miamala
yake anakuwa huru kwasababu tunajua Mwanafunzi anakuwa na mambo mengi vilevile
tunafahamu uchumi wa Mwanafunzi ndio maana tumeweza kuja na hii ili kuweza
kupunguza chaji za mwezi za makato, Akauti hii pia Mwanafunzi anaweza kuitumia
mahali popote ata akiwa tayali ameajiriwa” Alifafanua Isabela.
Akizungumzia manufaa yatokanayo na akaunti hiyo ya SCHOLAR Isabela amesema
kuwa inaweza kumsaidia Mwanafunzi kupata mkopo wa awali kupitia Benki ya CRDB
ili aweze kutatua changamoto zinazomkabili na kuweza kulipa pale atakapo pata
mkopo kutoka Bodi ya mikopo ya Elimu ya juu.
“Vilevili utaweza kupata huduma mbalimbali kupitia benki yetu ya CRDB kama
Simu benking,internet benking, na kuweza kufanya manunuzi ya mtadaoni ukiwa Chuoni
na unamkopo ni vizuri kujiifadhia fedha kidogo unapo maliza Chuo anagalau na wewe
unakuwa na fedha ambazo utaweza kuanzia
maisha mtaani ”.Aliongeza Meneja huyo wa CRDB Tawi la SUA.
Akiongea kwa niaba ya wanafunzi ambao wameshinda zawadi hizo Megan Manase
Mushi wamesema kupata Tanakilishi (Laptop) zitawasaidia katika kufanyia
shughuli mbalimbali za kimasomo maana hawakuwa nazo kabisa hivyo CRDB imekuwa
mkombozi katika kuwapatia vitendea kazi hivyo.
Paia wamewataka Wanafunzi wengine kujiunga na Benki ya CRDB kwani kwani imekuwa ina huduma nyingi nzuri kwaajili ya wanafunzi ambazo zitawasaidia katika kutunza fedha na kuzitumia vizuri pindi wanapozihitaji maana kila mahali sasa wanapatikana.
No comments:
Post a Comment