Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Bw. Richard Kwitega akifungua semina ya wahariri wa vyombo mbalimbali mbali mbali vya habari mkoani Arusha kuhusu Mfumo wa Ukusanyaji Mapato Serikalini (GePG), iiliyoanza leo katika ukumbi wa jengo la hazina ndogo lililo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango leo Februari 3,2021 ambapo mada mbalimbali zitatolewa na wataalamu wa mfumo huo na kuwajengea uelewa wahariri namna ya kuripoti habari zinazohusu mfumo huo.
Mkurugenzi wa Mifumo ya Kifedha kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. John Sausi akielezea kuhusu Mfumo wa Ukusanyaji Mapato Serikalini (GePG), iiliyoanza leo katika ukumbi wa jengo la hazina ndogo lililo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango leo Februari 3,2021 ambapo mada mbalimbali zitatolewa na wataalamu wa mfumo huo na kuwajengea uelewa wahariri namna ya kuripoti habari zinazohusu mfumo huo.
Mkurugenzi wa Mifumo ya Kifedha kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. John Sausi akifafanua zaidi kuhusu mifumo hiyo ya ukusanyaji malipo ya serikali.
Neema Maregeli Mchumi Mwandamizi Wizara ya Fedha na Mipango akielezea namna mfumo wa GePG unavyofanya kazi wakati wa semina hiyo inayofanyika kwenye ukumbi wa Wizara ya Fedha mkoani Arusha.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Benny Mwaipaja akitambulisha viongozi mbalimbali na maofisa wa Wizara ya Fedha pamoja na wahariri wa vyombo vya habari.
Baadhi ya wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini wakimsikiliza Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Bw. Richard Kwitega wakati akizungumza katika ufunguzi wa semina hiyo inayoendelea kwenye ukumbi wa Hazina ndogo Jijini Arusha.
Baadhi ya wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini wakimsikiliza Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Bw. Richard Kwitega wakati akizungumza katika ufunguzi wa semina hiyo inayoendelea kwenye ukumbi wa Hazina ndogo Jijini Arusha.
Picha mbalimbali zikionesha wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wakifuatilia ufunguzi wa semina hiyo inayofanyika kwenye ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango jijini Arusha.
Cynthia Mwilolezi kutoka Gazeti la Nipashe na Khalfan Sais wa KVIC Media wakifuatilia ufunguzi wa mkutano huo.
Mhariri Mkuu kutoka kituo cha matangazo cha Redio5 Arusha Bi. Ashura Mohamed akifuatilia mada kwa umakini katika semina ya siku mbili ya wahariri wa vyombo vya habari nchini inayoendelea jijini Arusha.
Jenipher Rauya Mchumi kutoka Wizara ra Fedha akiwa katika semina hiyo.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Benny Mwaipaja akijadiliana jambo na Neema Maregeli Mchumi Mwandamizi Wizara ya Fedha na Mipango.
Katibu Tawala mkoa wa Arusha Bw. Rchard Kwitega katikati,Mkurugenzi wa mifumo ya kifedha kutoka wizara ya fedha na mipango, Bw. John Sausi kushoto na Mwenyekiti wa Semina hiyo Benny Mwang'onda wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa semina hiyo mara baada ya kufunguliwa rasmi.
..........................................
Katibu tawala mkoa wa Arusha Bw. Richard Kwitega amesema kuwa Mfumo wa ukusanyaji wa fedha unapoboreshwa unawezesha nchi hukusanya kiasi kikubwa cha mapato ya ndani na kwa ufanisi mkubwa na kupelekea kurahisisha utekelezaji wa miradi mbali mbali ya maendeleo nchini.
Akifungua Semina ya Siku Mbili kwa Wahariri wa Vyombo vya habari nchini iliyoanza leo Mkoani Arusha, kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James, amesema kuwa Mfumo huu wa GePG ulianzishwa nchini kwa lengo la kuboresha ukusanyaji wa mapato kutokana na changamoto mbali mbali ambazo zilikuwepo ikiwemo gharama kubwa za miamala ya fedha za umma ikiwa ni pamoja na mlolomgo mzima wa utaratibu usio rafiki wa mlipaji huduma za umma na namna ya anavyopatiwa Ankara,jinsi anavyolipa Ankara,na jinsi anavyopatiwa Stakabadhi yake.
Aidha Bw. Kwitega amesema kuwa mfumo ambao ulikuwa unatumika awali ulikuwa hauwezi kukupa taarifa sahihi na kwa wakati wa makusanyo na kwa uwazi unaotakikiwa.
Mfumo huo wa GePG umeunganishwa na taasisi zipatazo 670 kutoka katika maeneo mbali mbali ikiwemo Serikali za mitaa, Halmashauri, Taasisi nyingine pamoja na serikali kuu.
Katika kuepuka matumizi mabaya ya pesa za serikali Watanzania wametakiwa kuanza kutumia mfumo mpya wa serikali wa kulipia huduma mbali mbali (GePG) ili kuepuka fedha rushwa na malipo yao kushindwa kufika serikalini.
Nae Mkurugenzi wa mifumo ya kifedha kutoka wizara ya fedha na mipango, Bw. John Sausi amesema kuwa wakati umefika sasa kwa watanzania Kutumia mfumo huo ili kuwa na uhakika wa malipo yao.
“Ndugu zangu wahariri naomba mtumie fursa mlizo nazo katika kuhakikisha kuwa mnaelimisha watazania kuhusu umuhimu wa kutumia mfumo huu wa GePG ili fedha zenu mnazolipa kupitia ‘CONTROL NUMBER” mnazopewa kufika moja kwa moja serikalini, na pili inaiwezesha serikali kuona mapato yote kupitia mfumo huu na kuhakikisha fedha za umma hazipotei,”alisema Bw. Sausi
Hata hivyo Bw. John Sausi amewataka watanzania kuhakikisha wanaepuka kulipa pesa taslimu kwa kuwa mfumo huo umeshapitwa na wakati na fedha hizo hazifiki kwa wakati na huenda zinaweza kupotea na kusababisha hasara kwa mwananchi.
Pia ametaja mafanikio yaliyopatikana kupitia mfumo wa GePG ni kuokoa fedha nyingi za serikali ambazo zimekuwa zikipotea kabla ya mfumo huu na pia kuiwezesha serikali kupata na kuona taarifa mbali mbali zinazohusu ukusanyaji wa mapato nchini.
No comments:
Post a Comment