TIGO KUWAPA WATEJA DAKIKA 10 BURE KILA SIKU - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday 10 February 2021

TIGO KUWAPA WATEJA DAKIKA 10 BURE KILA SIKU

 

Woinde Shisael-Meneja Mawasiliano  Tigo, akitambulisha ofa mpya inaiyoitwa Amka na Tigo, ambayo itampa mteja dakika 10 za kupiga bure kila siku kuanzia saa kumi na asubuhi hadi saa tatu. kushoto kwake Ndevonaeli Eliakimu - Meneja kitengo cha Biashara Tigo.


Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya simu za mkononi ya Tigo, leo inayo furaha kutambulisha huduma mpya ya Amka na Tigo.

Huduma hii itakua ikimpa fursa mteja wa Tigo kupiga simu  bure katika mipango yake ya kila siku asubuhi.

Kila mteja wa Tigo atakua akipokea dakika 10 za bure kupiga simu za Tigo kwenda Tigo kuanzia saa 12:00 asubuhi hadi saa 3:00 asubuhi.

Hii ni ofa maalumu kwa wateja wa Tigo kwa ajili ya kuhakikisha wanakamilisha mipango yao pamoja na wapendwa wao.

Akizungumza Dar es Salaam, Meneja Mawasiliano kutoka Tigo, Woinde Shisael, alisema, “Tunataka kurudisha kwa wateja wetu ambao tumekuwa nao kwa kipindi chote kile tunachokipata.
 
"Tunaamini kila mteja wetu ni muhimu kwetu, ofa hii itasaidia kuimarisha mawasiliano baina ya wateja wetu na familia zao, marafiki na wanaofanya nao biashara kila siku asubuhi na mapema.

“Tigo ni chapa ambayo inaelewa mahitaji ya wateja wake na tunaamini Amka na Tigo itasaidia kila mteja wa Tigo kufanya mawasiliano kwa uhakika," alisema Shisael.

Tigo daima imekuwa ya kwanza kuuza na kutoa suluhisho za ubunifu zinazoleta mabadiliko mazuri  sokoni.

Alisema Amka na Tigo itawezesha wateja wote wa Tigo, kwani watu wengi hupanga siku yao asubuhi kwa kuzungumza na familia, marafiki na wafanyabiashara.

"Kwa miaka mingi Tigo Tanzania imeanzisha ubunifu kama vile Facebook ya bure kwa Kiswahili, simu mahiri za Kiswahili, kwa lengo la kuondoa vizuizi vya mawasiliano kati ya wateja wake. Sasa, pamoja na Amka na Tigo, zaidi ya wateja wa Tigo milioni 12 wataweza kuamka na kupiga simu za bure bila wasiwasi wa kuwa na muda wa maongezi katika simu zao. Hii inadhihirisha juhudi zetu katika kuwa huduma inayowapa wateja wetu dhamana ”. alifafanua Shisael.

Alisema siku nzuri huanza kwa kupanga mapema, piga simu za bure za Tigo kwenda Tigo kutoka saa 12 asubuhi hadi saa 3 asubuhi na Amka na Tigo. Hakuna usajili unaohitajika

No comments:

Post a Comment