TADB YAWEZESHA WAFUGAJI KUPATA NG'OMBE WA KISASA WA MAZIWA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday, 1 February 2021

TADB YAWEZESHA WAFUGAJI KUPATA NG'OMBE WA KISASA WA MAZIWA


Meneja wa Kanda ya Mashariki wa Benki ya Kilimo (TADB) Jeremiah Mhada wa kwanza kulia akimkabidhi hundi ya Sh Milioni 396 Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki kwa ajili ya wafugaji mkoani Tanga kupata mbegu ya ng’ombe bora wa kisasa wa maziwa wakiwemo wafugaji 114 kupitia vyama vya msingi 5 kupata mikopo ya ng’ombe wa kisasa wa kwanza kushoto anayshuhudia ni Kaimu Msajili bodi ya maziwa Noely Byamungu.

Meneja wa Kanda ya Mashariki wa Benki ya Kilimo (TADB) Jeremiah Mhada wa kwanza kulia akimkabidhi hundi ya Sh Milioni 396 Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki kwa ajili ya wafugaji mkoani Tanga kupata mbegu ya ng’ombe bora wa kisasa wa maziwa wakiwemo wafugaji 114 kupitia vyama vya msingi 5 kupata mikopo ya ng’ombe wa kisasa wa pili kushoto anayeshuhudia ni Kaimu Msajili bodi ya maziwa Noely Byamungu.
 
Meneja wa Kanda ya Mashariki wa Benki ya Kilimo (TADB) Jeremiah Mhada akizungumza wakati wa halfa hiyo.

Sehemu ya wafugaji wakimsikiliza Meneja wa Kanda ya Mashariki wa Benki ya Kilimo (TADB) Jeremiah Mhada akizungumza wakati wa halfa hiyo.

BENKI ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imekwisha toa mikopo yenye thamani ya Shilingi billioni 11.80 ili  kuwezesha mnyororo wa thamani wa sekta ya maziwa kote nchini.

Pia imewezesha wafugaji mkoani Tanga kupata mbegu ya ng’ombe bora wa kisasa wa maziwa wakiwemo wafugaji 114 kupitia vyama vya msingi 5 kupata mikopo ya ng’ombe wa kisasa wenye thamani ya Zaidi ya Tsh 396m.

Akizungumza katika hafla iliyoandaliwa na shirika la kimataifa la Heifer, Meneja wa Kanda ya Mashariki wa Benki ya Kilimo (TADB) Jeremiah Mhada alieleza umuhimu wa ushirikiano wa wadau muhimu katika sekta ya mifugo ili kuongeza tija nakuleta mapinduzi ya kweli katika sekta ya maziwa nchini.

Alisema  kupitia mkopo huu, TADB imeweza kuwajengea wafugaji hao mabanda ya kutunzia ng’ombe 25 na kupata mitamba ya kisasa ili wanufaike na ufugajiwa ng’ombe wa maziwa ikiwemo kupatiwa mikopo naafuaa itakayowawezesha kupata mbegu bora za ng'ombe wa maziwa.

 “TADB ili kuhakikisha wafugaji wananufaika na sekta hii ya maziwa tuliingia katika ushirikiano na shirika la kimataifa la Heifer International kuhakikisha wafugaji wetu wanajengewa uwezo wa namna bora ya ufugaji wa ng’ombe wa maziwa lakini pia kujiunga katika vikundi ili kuweza kupata mikopo kwa urahisi.”Alisema

TADB imewezesha vyama vya msingivya UWAMWA, CHAWAMU, UWAKO, UWAMKI na UWADAKI kuweza kupata jumla ya ng’ombe wa kisasa 156 kwa wafugaji 121 ikiwemo wanawake 39 pamoja na kuwawezesha kupata mkopo huo wafugaji hao tayari wana soko la kuuza maziwa yao.

"Kwa hapa Tanga wataweza kuuza kwa kampuni ya Tanga Fresh ambayo nayo TADB imekwisha iwezesha katika kumudu kuweza kununua maziwa kutoka kwa wafugaji hawa wadogowadogo.” Alisisitiza Mhada.

Kabla ya kufanya makabidhiano hayo,TADB kwa kushirikiana na Shirika la kimataifa la Heifer International waliendesha mafunzo kwa viongozi wa vyama vya ushirika 26 ambao walijengewa uwezo kwenye namna ya usimamizi bora wa biashara, usimamizi wa fedha, utunzaji wa kumbukumbu, utunzajiwa kumbukumbu na uongozi bora.

“Ufugaji ili uwe na tija nilazima wafugaji wajengewe uwezo na ni muhimu kufahamu namna ya kusimamia fedha, utunzaji wa kumbukumbu,uongozi bora na masuala mengine ya usimamizi wa biashara kwa kuwa na uwezo huu, mfugaji anaweza kuona namna anavyonufaika na mkopo na hata kuweza kufahamu kipato chake.”Aliongezea Mhada.

Alisema Wafugaji wadogo kupitia TADB wanaendelea kunufaika na fursa zilizopo kupitia benki ya kilimo na pia kupitia ushirikiano huo wa TADB nashirika la kimataifa la Heifer.
 
Serikali imeainisha sekta ya maziwa kama moja ya sekta muhimu katika kuchochea uwekezaji katika viwanda jambo ambalo TADB inawawezesha wawekezaji kama kampuni za Tanga Fresh, Kahama Fresh, Njombe Milk na viwanda vingine katika maeneo mbalimbali nchini.

Aliongeza kwamba kupitia uwekezaji katika mnyororo wa thamani wa sekta ya kilimo, pia kama Taifa wanaweza kujihakikishia upatikanaji na usalama wachakula,lishe bora na kipato kwa wafugajina pia kuongezapato la Taifa.

Mhada alisema sekta  ya maziwa nchini inachangia asilimia 1.2% yapato la Taifa huku akieleza ili kuhakikisha wanaongeza kipato kwa wafugaji wadogo wadogo ambao kupitia shughuli hizi za ufugaji huchangia pato la Taifa.
Alisema wamewezesha kupata mitamba ya kisasa na kuwaunganisha na masoko ili kuongeza thamani na kuchochea ongezauzalishaji wa mazi wa nchini.

No comments:

Post a Comment