RUWASA RUVUMA ILIVYODHMIRIA KUSAMBAZA MAJI VIJIJINI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Saturday, 20 February 2021

RUWASA RUVUMA ILIVYODHMIRIA KUSAMBAZA MAJI VIJIJINI

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme akifurahi mradi wa maji katika kijiji cha Mkongo wilayani Namtumbo uliosimamiwa na RUWASA.

Mradi wa maji uliosimamia na RUWASA katika eneo la Nandembo Wilayani Tunduru.

WAKALA wa Maji na Usafi wa Mazingira vijijini (RUWASA) ilianzishwa kwa Sheria namba tano ya huduma ya maji na usafi wa mazingira ya mwaka 2019 na kuanza kutumika rasmi Julai Mosi, 2019.

Mhandisi Rebman Ganshonga ni Meneja wa RUWASA Mkoa wa Ruvuma, anabainisha utekelezaji wa miradi ya maji na mwelekeo wa RUWASA mkoani Ruvuma katika utoaji huduma ya maji vijijini.

Mhandisi Ganshonga anataja hali ya upatikanaji huduma ya maji kwa kila Halmashauri hadi kufikia Juni 2019, ambapo Halmashauri ya Wilaya ya Songea yenye watu 141,427, idadi ya watu wanaopata huduma ya maji ni 86,270 sawa na asilimia 61.0 na kwamba Halmashauri hiyo ina vituo vinavyotoa maji 951 kati ya hivyo vinavyofanyakazi ni vituo 590.

Kwa mujibu wa Mhandisi huyo, katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea RUWASA inahudumia wakazi 90,730, watu wanaopata huduma ya maji ni 45,479 sawa na asilimia 50.0 ambapo idadi ya vituo vya kutolea maji ni 401 kati ya hivyo vituo vinavyofanya kazi ni 372.

“Katika Halmashauri ya Mbinga yenye idadi ya watu 235,648, idadi ya watu wanaopata maji ni 123,648 sawa na asilimia 52.4, idadi ya vituo vya kuchotea maji ni 375, vituo vinavyofanya kazi ni 196’’, anasema Mhandisi Ganshonga.

Kulingana na Meneja huyo,katika Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo yenye wakazi  226,945, idadi ya watu wanaopata huduma ya maji ni 147,515 sawa na asilimia 65.0 na kwamba kuna vituo 939 vya kuchotea maji, kati ya hivyo vituo vinavyofanyakazi ni 484.

Anabainisha zaidi kuwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru yenye wakazi 256,510, watu wanaopata huduma ya maji ni 164,166 sawa na asilimia 64.0 na kwamba katika Halmashauri hiyo vimejengwa vituo vya kuchotea maji 954 kati ya hivyo vinavyofanyakazi ni 714.

Kwa mujibu wa Meneja RUWASA Mkoa, katika Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa yenye wakazi146,160,watu wanaopata huduma ya maji ni 73,080 sawa na asilimia 50.0 na kwamba vituo vya kuchotea maji ni 645 kati ya hivyo vinavyofanya kazi ni 312.

Katika Halmashauri ya Madaba yenye wakazi 53,883, idadi ya watu wanaopata huduma ya maji ni 33,407 sawa na asilimia 62.0 na kwamba Halmashauri hiyo ina vituo vya kuchotea maji 419, kati ya hivyo vituo vinavyotoa maji ni 267.

Kulingana na Mhandisi Ganshonga,katika Halmashauri ya Mbinga Mji yenye wakazi 68,338, idadi ya watu wanaopata maji ni 32,500 sawa na asilimia 47.7 na kwamba katika Halmashauri hiyo kuna vituo 305 vya kuchotea maji kati ya  hivyo ni vituo vinavyofanyakazi ni 130.

“Kwa ujumla katika Mkoa wa Ruvuma RUWASA inahudumia wakazi 1,219,642, kati yao idadi ya watu wanaopata maji ni 704,065 sawa na asilimia 57.9, jumla ya vituo vya kuchotea maji ni 4,989, vituo vinavyofanyakazi ni 3065’’, anasisitiza Mhandisi Ganshonga.

Hata hivyo anaitaja hali ya upatikanaji wa maji katika Halmashauri zote nane mkoani Ruvuma hadi kufikia Desemba 2020 iliwezesha wakazi 833,361 kati ya 1,344,397 kupata maji  sawa na asilimia 62.6.

Anaitaja bajeti ya RUWASA mkoani Ruvuma katika kipindi cha  mwaka wa fedha 2020/2021 imelenga kutekeleza idadi ya miradi ya maji 77  katika Wilaya za Songea, Mbinga, Namtumbo, Tunduru na Nyasa ambapo jumla ya shilingi bilioni 17,095,079,568.15 zimetengwa.


No comments:

Post a Comment