RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA RASMI DARAJA LA JUU LA UBUNGO (KIJAZI INTERCHANGE) - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya

Wednesday, 24 February 2021

RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA RASMI DARAJA LA JUU LA UBUNGO (KIJAZI INTERCHANGE)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kufungua Daraja la Juu katika Makutano ya Barabara za Ubungo (Kijazi Interchange) Ubungo jijini Dar es Salaam leo, wengine ni viongozi wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, TANROADS na Mkoa wa Dar es Salaam.

Muonekano wa Daraja la Juu la Ubungo Interchange ambapo kwasasa linaitwa Kijazi Interchange mara baada ya kuzinduliwa jijini Dar es Salaam.

Muonekano wa Daraja la Juu la Ubungo Interchange ambapo kwasasa linaitwa Kijazi Interchange mara baada ya kuzinduliwa jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (sekta ya Ujenzi) Arch. Elius Mwakalinga akiteta jambo na Naibu Waziri, Godfrey Kasekenya katika hafla ya uzinduzi wa Daraja la Juu la Ubungo Interchange sasa Kijazi Interchange.

Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Mhe. Godfrey Kasekenya, Katibu Mkuu (sekta ya Ujenzi) Arch. Elius Mwakalinga na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Eng. Patrick Mfugale wakisalimiana walipokutana katika hafla ya uzinduzi wa Daraja la Juu la Ubungo Interchange sasa Kijazi Interchange.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Abubakari Kunenge (kulia) akisisitiza jambo kwa viongozi wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi katika hafla ya uzinduzi wa Daraja la Juu la Ubungo Interchange sasa Kijazi Interchange.

Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Mhe. Godfrey Kasekenya, Katibu Mkuu (sekta ya Ujenzi) Arch. Elius Mwakalinga na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Eng. Patrick Mfugale wakisalimiana walipokutana katika hafla ya uzinduzi wa Daraja la Juu la Ubungo Interchange sasa Kijazi Interchange.

Wafanyakazi wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), wakifurahia jambo kabla ya uzinduzi wa Daraja la Juu la Ubungo Interchange sasa Kijazi Interchange.

Muonekano wa Daraja la Juu na barabara ya chini Ubungo Interchange ambapo kwasasa linaitwa Kijazi Interchange.

Wafanyakazi wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), wakifuatilia hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa uzinduzi wa Daraja la Juu la Ubungo Interchange sasa Kijazi Interchange.

Baadhi ya Watendaji wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi wakifuatilia hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa uzinduzi wa Daraja la Juu la Ubungo Interchange sasa Kijazi Interchange.

No comments:

Post a Comment