TUTATENGA FEDHA KWA AJILI YA HUDUMA ZA UGANI - PROF. MKENDA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Sunday, 31 January 2021

TUTATENGA FEDHA KWA AJILI YA HUDUMA ZA UGANI - PROF. MKENDA

 

Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda akitoa hotuba ya kufunga kikao kazi cha siku mbili cha wataalam wa kilimo toka mikoa na halmashauri zote 185 jana ukumbi wa LAPF Dodoma ambapo amesema wizara yake katika bajeti ijayo itatenga fedha kwa ajili ya kuboresha huduma za ugani ili kukuza tija ya uzalishaji.


Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya akiwa ameshika kijitabu kinachoonyesha Tozo, Ada na Kodi 105 zilizofutwa na Serikali ya Awamu ya Tano katika Bodi na Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Kilimo mwaka 2015-2020 ili kuondoa kero kwa wakulima na wawekezaji.Wizara imegawa nakala za vijitabu hivyo kwa Maafisa Kilimo Mikoa  26 na Halmashauri zote 185 jana Dodoma ili wakaeleze mafanikio hayo kwa wakulima.


Sehemu ya Maafisa Kilimo toka mikoa na Halmashauri zote nchini wakiwa kwenye kikao kazi na Waziri wa Kilimo kujadili upatikanaji huduma za ugani jana ukumbi wa LAPF Dodoma.

No comments:

Post a Comment