Afisa Uhusiano wa Tanga Uwasa Devotha Mayalla akieleza jambo wakati wa mkutano huo. |
Mkazi wa Mtaa wa Kange Kasera Kata ya Maweni Seba akiuliza swali katika mkutano huo. |
Hayo
yalibainishwa na Mkuu wa Kitengo cha Mipango na Ujenzi wa Tanga Uwasa
Mhandisi Salum Ngumbi wakati akizungumza wakati akitoa elimu kwa
wananchi wa mtaa wa Kange Kasera Kata ya Maweni Jijini Tanga.
Elimu
hiyo ambayo ilitolewa wakati wa mkutano huo imekuwa endelevu kuweza
kukutana na wananchi kusikiliza kero zao na namna ya kuweza kuzipatia
ufumbuzi ambao ulifanyika shule ya Msingi Kasera.
Alisema
kwa sasa Tanga Uwasa wanazalisha maji mita za ujazo elfu 30 kwa siku
lakini mahitaji ya wananchi kwa siku ni mita za ujazo elfu 35 kwa siku.
“Kutokana
na hilo ndio maana tumepanga kufanya mradi wa kuongeza miuondombinu ya
kuzalisha maji kutoka mita za ujazo elfu 30 mpaka elfu 45 kwa siku na
mradi huo utaanza mwezi Aprili mwaka huu”Alisema
Mhandisi
Salum alisema mradi huo utakuwa wa miezi 12 na utakuwa na manufaa
makubwa mawili katika mji wa Tanga la kwanza wananchi upatikanaji wa
maji ya uhakika ambayo hayakatikikatiki na maji yatapatikana maeneo yote
masaa 24.
Alisema pia
wakati wa utekelezaji mradi vijana watanufaika kwa sababu watakwenda
kuongeza machujio mawili kwenye mtambo wa kusafishia maji uliopo mowe
Pande.
Aidha alisema
hivyo kazi ya ujenzi kubwa itafanyika na kuna tenki la kuhifadhi maji
lenye ujazo wa lita milioni 1 na watakwenda kujenga jengine lenye ujazo
wa lita milioni 1 eneo la Pande .
Mhandisi
huyo alisema pia watalaza bomba kubwa lenye kipenyo cha milimita 600
kwa urefu wa kilomita 12.5 kutoka mowe mpaka Kange Jeshini na kwenye
tenki hilo bomba litakuwa na kazi ya kusafirisha maji wanayoyazalisha
na watakiwa na mabomba mawili makubwa ya kupelekea maji Tanga.
“Hivyo vijana watanufaika kwenye kazi za ujenzi kuchimba mitaro kwani
kwenye mikataba ambayo wataingia na wakandarasi kwamba kazi yoyote
ambayo haihitaji wataalamu maalumu inatakiwa itoke sehemu ya mradi kata
ya maweni inaguswa kwa eneo la Mkurumuzi mpaka kange Jeshini," Alisema.
Aliwataka vijana wajitokeza kwa wingi kupata hiyo ajira ya muda hivyo tunawaomba
wananchi kuwa tayari kupokea mradi na kutoa ushirikiana na mradi mkubwa
una thaman i ya Bilioni 8.4 na wanasoimamia wenywe wataalamu wa Tanga
Uwasa
Awali akizungumza
katika mkutano Afisa Uhusiano wa Tanga Uwasa Devotha Mayala hivi sasa
wamekuwa wakijitahaidi kadri wawezavyo kuboresha huduma zao na sasa
hawana utaratibu mpaka mteja kufika ofisini kwao wanatumia simu zao
wanapata huduma.
Alisema
walichokwenda kuzungumza nao leo ni kutambulisha mradi mkubwa wa kutanua
mtambo wa kuzalisha na kutibu maji wa Mowe ambapo maeneo yote ya kata
za Maweni na Kiomoni yataguswa moja kwa moja na huo mradi.
No comments:
Post a Comment