KUAPISHWA KWA JOE BIDEN: BIDEN AWA RAIS WA 46 WA MAREKANI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday 21 January 2021

KUAPISHWA KWA JOE BIDEN: BIDEN AWA RAIS WA 46 WA MAREKANI

 





JOE Biden amekula kiapo na kuwa rais wa 46 wa taifa la Marekani. Biden amekula kiapo mbele ya jaji wa Mahakama Kuu John Roberts. Baada ya kula kiapo Biden amelihutubia taifa kwa mara ya kwanza akiwa Rais wa Marekani akisema ''hii ni siku ya kidemokrasia''. Siku ya kihistoria na matumaini.

"Marekani imejaribiwa na kunyanyuka tena dhidi ya changamoto. Leo tunasheherekea ushindi si wa mgombea isipokuwa ushindi wa demokrasia,".

"Ninawashukuru watangulizi wangu wa vyama vyote walio hapa hii leo," alisema Rais mpya. Marais wa zamani Clinton, Bush na Obama wamehudhuria sherehe hiyo. Biden amesema alizungumza kwa njia ya simu na Rais Jimmy Carter- ambaye sasa ana miaka 96, na kumpongeza kwa utumishi wake.

Mtangulizi wake, Donald Trump hajahudhuria tukio hilo muhimu, na hatua hiyo imemfanya kuwa rais wa kwanza kutohudhuria sherehe za kuapa kwa mrithi wake tangu mwaka 1869.

Rais mpya ametangaza msururu wa maagizo yanayolenga kugeuza sera kuu za Bw Trump.

Makamu wa Rais mteule Harris aliapishwa mbele ya Bwana Biden - kuwa mwanamke wa kwanza na mtu wa kwanza mweusi na mwenye asili ya Asia na Amerika aliyeinuliwa kuhudumu katika nafasi ya pili muhimu baada ya Urais.

Shughuli za uapisho zimefanyika wakati kukiwa na ulizi mkali baada ya waandamanaji wanaomuunga mkono Trump kufanya vurugu tarehe 6 mwezi Januari.

Wanajeshi 25,000 wanalinda eneo linalofanyika sherehe hizo, sherehe ambazo zimekosa kuhudhuriwa na maelfu ya watu kama ilivyo desturi yake kwa sababu ya janga la corona.

Mapema Jumatano Bw Biden alihudhuria Misa katika kanisa kuu huko Washington - pamoja na viongozi wanne wa baraza kuu la Katoliki, wote wa Democratic na Republican - kabla ya kwenda Capitol. Akiwa na umri wa miaka 78, Bwana Biden ndiye rais wa Marekani mwenye umri mkubwa zaidi kuwahi kuapishwa.

Makamu wa Rais anayemaliza muda wake Mike Pence pia amehudhuria sherehe hiyo. Hakwenda kwenye hafla ya salamu ya kijeshi ya Bwana Trump katika uwanja wa Andrews.

Awali wasaidizi walisema Bw Biden atatumia hotuba yake kutoa wito wa matumaini wa umoja wa kitaifa baada ya utawala wa mtangulizi wake kutoka chama cha Republican. Sherehe hizo zilipambwa na watumbuizaji kama vile Lady Gaga- aliyeimba wimbo wa taifa, halikadhalika Jenifer Lopez na Garth Brooks.

Tamasha la jioni litahodhiwa na Tom Hanks na Bruce Springsteen, John Legend, Jon bon Jovi, Justin Timberlake na Demi Lovato.

Katika hotuba yake katika kambi ya kijeshi ya Andrews Air Force , rais anayeondoka aliangazia kile alichokitaja kuwa ufanisi wa utawala wake kama rais.

Bwana Trump mwenye umri wa miaka 74 aliondoka ili kuanza maisha ya bila urais katika uwanja wa mchezo wa gofu huko Mar-a lago katika ufukwe wa bahari wa Palm Beach. Katika saa zake za mwisho katika madaraka bwana Trump aliwapatia uhuru zaidi ya watu 140 , akiwemo mshauri wake wa zamani Steve Bannon , ambaye alikabiliwa na mashtaka ya kufanya udanganyifu.

Matukio ya kisiasa yanayomzunguka hayajaisha. Bunge la Seneti linatarajiwa kumshtaki kufautia kushtakiwa na bunge la uwakilishi kwa mara ya pili kwa kuchochea ghasia za Capitol.

Siku ya Jumanne , Kiongozi wa Republican katika bunge la seneti Mitch McConell , alisema kwamba waandamanaji hao walichochewa na rais Trump na kuambiwa uongo.

No comments:

Post a Comment