WANAARUMERU JENGENI MAZOEA YA KUPIMA AFYA ZENU MBUNGE ZAITUN SWAI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Saturday, 12 December 2020

WANAARUMERU JENGENI MAZOEA YA KUPIMA AFYA ZENU MBUNGE ZAITUN SWAI

Zaitun Swai akipima Shinikizo la damu ikiwa ni ishara ya uzinduzi waupimaji wa Afya bure kwa Wakazi wa wilaya ya Meru mapema wilayani huo picha zote na Ahmed Mahmoud Arumeru.

Na Ahmed Mahmoud Arusha 

WAKAZI wilayani Arumeru wameaswa kupenda kupima Afya zao kwa lengo la kupambana na magonjwa yasioambukiza ambayo yamekuwa yakishika kasi nchini. Akiongea wakati akifungua zoezi la upimaji wa Afya ikiwemo saratani ya kizazi na mfumo wa hewa sanjari na uchangiaji wa Damu zoezi lililoandaliwa na kampuni ya Phide Entertainment ya jijini Arusha kwa kushirikiana na hospital yamkoa ya Mount Meru linalofanyika wilayani Arumeru kwa siku mbili. 

Mbunge wa viti maalumu mkoani hapa Zaytun Swai alisema kuwa umuhimu wa upimaji wa Afya kwa watanzania unahitajika kuwa utamaduni kama sehemu kubwa ya maisha yao kwa kupima na kutosubiri hadi unapozidiwa ndipo unaenda hospitali jambo linalopelekea usugu wa maradhi.

Alisema kuwa watanzania wakijenga utamaduni huo itakuwa ni kujenga Taifa imara kujengea na watu wenye Afya njema  itakuwa rahisi kuzijenga Afya zao na kuondokana na kusubiria hadi wanapokuwa kwenye hatua za mwisho za magonjwa na kupeleka kuzorota kwa Afya zao hivyo kupunguza nguvukazi ya kuleta maendeleo.

Akawataka wananchi wengi kujitokeza kwa wingi kupima Afya zao wakitambua ni mtaji wa kujiletea maendeleo na kulijenga Taifa lenye watu imara wenye Afya bora. Awali akimkaribisha mgeni Rasmi wa Ufunguzi huo Mkurugenzi wa Phide Entertainment Phide Mwakitalima alisema kuwa zoezi hilo la upimaji ni kwa siku mbili na watafanya kwa wilaya zote za mkoa wa Arusha lengo ni kuhakikisha wanajenga utamaduni wa wananchi kupenda kupima Afya zao bila kusubiria kuugua ndipo wapime 

Alisema kuwa msingi mkubwa kwa ni baada ya kuguswa na uhitaji wa wananchi na ndipo wakandaa zoezi hilo la upimaji wa bure wa Afya zao unaenda sambamba na uchagiaji wa damu ikiwa ni kuchangia benki ya damu ya mkoa.

Kwa Upande wake Mtaalamu wa Afya kutoka hospital ya Mount Meru Juma Muna Alitilia mkazo umuhimu wa uchangiaji wa damu kwani kumekuwa na mahitaji makubwa ya damu salama hususani hospitali ya mkoa inayohitaji kati ya chupa 300 hadi 400 huku mkoa ukihitaji chupa 900.

Alisema wananchi wengi wanahitajika kuona umuhimu wa uchangiaji wa damu kwenye benki yetu ya mkoa sanjari na upimaji wa Afya zao utakaosaidia kupambana na magonjwa yasioambukiza ambayo yanashamiri sana kwa miaka ya karibuni.

No comments:

Post a Comment